Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima amesema Ofisi ya Rais TAMISEMl inatarajia kuleta Timu kuchunguza Sakata la Uuzaji wa Viwanja namba 194 na 195 Katika Kitalu U kwenye Mtaa wa Rwegasore Jijini Mwanza ili kujiridhisha na taratibu zilizotumika pamoja na utendaji kwa ujumla wa Sekta ya Ardhi kutokana na uwepo wa malalamiko mengi kutoka kwa wananchi.
Mhe. Malima amesema hayo leo (Januari 26, 2023) wakati akipokea Ripoti Maalum kutoka kwa Timu aliyoiunda Januari 13, 2023 kuchunguza taratibu zilizotumika kuuza Viwanja hivyo licha ya uwepo wa zuio lililotolewa na Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Nyamagana kwenye kikao kilichoketi Septemba 28, 2022.
Aidha, ameishukuru Timu hiyo kwa kukamilisha kazi ndani ya muda waliopatiwa (Siku 7) na akabainisha kuwa Ofisi yake itawasilisha taarifa kwenye Ofisi ya TAMISEMl, Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU ili kuzitaarifu juu ya yaliyobanika kwenye uchunguzi uliofanywa na Kamati hiyo.
Awali, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mkurugenzi wa Maadili wa Kanda ya ziwa Ndugu Godson Kweka alifafanua kuwa katika kutekeleza jukumu hilo wameongozwa na Hadidu za rejea 11 zikiwemo kuchunguza Historia ya Umiliki wa viwanja hivyo, sababu zilizomfanya Mkurugenzi wa Jiji kuamua kuviuza pamoja na uwepo wa zuio la kufanya hivyo ambalo lilitolewa na Kikao ambacho naye alishiriki.
Zingine ni kuwachunguza watumishi walioshiriki katika Uuzaji wa viwanja hivyo, Ushiriki wa Kamishna Msaidizi wa Ardhi kwenye suala hilo, Uwezo wa Menejimenti ya Halmashauri hiyo katika kushauri mambo, thamani halisi ya viwanja hivyo na uchungu notzi dhidi ya washiriki wote hata amabo sio watumishi wa umma waliohusika kwenye mchakato wa kuuza viwanja hivyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.