TUENDELEE KUMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUTANUA WIGO WA AJIRA NCHINI: RC MTANDA
Mkoa wa Mwanza leo umesheherekea Sikukuu ya Wafanyajazi, Mei Mosi kwa kumshukuru Rais Samia kwa kuendelea kutanua wigo wa ajira kutokana na ujenzi wa miundombinu mbalimbali hapa nchini.
Akizungumza na wafanyajazi kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Said Mtanda amesema miradi mingi inayofanyika mkoani humo imetoa nafasi za ajira pamoja na kuwatengenezea vijana mazingira mazuri ya kujiajiri.
"Mradi kama wa Daraja la JP Magufuli umetengeneza ajira 1875, hali ambayo imesaidia kuongezeka vipato kwa familia na kupunguza idadi ya vijana kukaa vijiweni kutokana na kukosa kazi",amesema Mkuu huyo wa Mkoa.
Amesema Serikali ya awamu ya Sita imekuwa na sikio kwa Shirikisho la Wafanyajazi TUCTA kwa kuongeza mishahara huku ikitenga bajeti kwa ajili ya kuwatengenezea vijana mazingira ya kujiajiri.
Akizungumzia kauli mbiu ya mwaka huu isemayo nyongeza ya mishahara ni msingi wa mafao bora na Kinga dhidi ya hali ngumu za maisha,Mtanda amebainisha ni sahihi wafanyajazi kuwa na maslahi bora lakini siku zote mshahara huwa hautoshi.
"Natoa rai kwa wafanyajazi wenzangu tujenge utamaduni wa kubuni vyanzo vya mapato halali kama ni kilimo au ufugaji,hii itasaidia kuongeza vipato kwenye familia zetu",Mkuu wa Mkoa.
Mratibu wa Sherehe za Mei Mosi Mkoani Mwanza Halfan Nyungwa amebainisha bado baadhi ya Taasisi binafsi zimekuwa Waziri kuwasilisha michango ya Wafanyajazi hali ambayo inaleta usumbufu na mlomlongo wa kesi za madai kwenye tume zinazoshughulika na migogoro ya Wafanyajazi.
"Tunaiomba Serikali iangalie upya Sheria kwenye mifuko ya Jamii,bado inaonesha haina nguvu ya kutosha kushughulika na Taasisi zinazozembea kuwasilisha michango ya Wafanyajazi",Mratibu wa Sherehe.
Sherehe hizo zilizofanyika Ki-mkoa Wilayani Ilemela,zimekwenda pamoja na kukabidhiwa zawadi kwa baadhi ya Wafanyajazi bora.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.