TUENDELEE KUSHIKAMANA WANA MWANZA PAMBA JIJI FC ITIMIZE LENGO LA KUCHEZA LIGI KUU MSIMU UJAO-RC MAKALLA
*Asema siri ya kufikia malengo ni mshikamano wa pamoja kutoka kwa mashabiki
*Aonesha matumaini ya kucheza Ligi kuu kutokana na ubora wa Pamba Jiji FC
Wakati wana TP Lindanda wakiendelea kung'ara kwa mfululizo wa ushindi michuano ya soka Ligi ya Championship kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Pan African,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza CPA Amos Makalla ameendelea kuwaomba mashabiki wa soka kuendelea kuipa ari timu hiyo kwa kufurika uwanjani katika kila michezo ya timu hiyo.
Mkuu huyo wa Mkoa ambaye pia ni mlezi wa timu biyo akizungumza na vyombo vya habari leo kwenye uwanja wa Nyamagana mara baada ya mpambano,amesema huu ni mwanzo mzuri ambao unaleta matumaini ya kucheza Ligi kuu msimu ujao.
"Siku zote shabiki uwanjani ni mchezaji wa 12 hivyo napenda kuwaomba tuendelee kushikamana kwa pamoja kwa lengo la kuwatia moyo wachezaji wetu wazidi kufanya vizuri,"Mhe.Makalla
Mhe.Makalla amebainisha Ligi ya Championship ni ngumu kutokana na timu zinazopambana kupanda Ligi kuu ni nyingi na zenye uwezo,hivyo wajibu wa kila mwana Mwanza ni kuwaunga mkono wana TP Lindanda.
Katika mchezo huo Pamba Jiji FC walilazimika kupata ushindi huo muda wa lala salama kwa mkwaju wa penati uliofungwa na mchezaji Jamal Mtegeta na kuamsha shamra shamra na nderemo kutoka kwa mashabiki waliofurika uwanjani hapo.
Mara baada ya filimbi ya mwisho kuashiria kuhitimisha mpambano huo,mlezi wa timu hiyo akiongozona na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe.Amina Makilagi,Mbunge wa Jimbo la Nyamagana,Mhe.Stanslaus Mabula na Meya wa Jiji Mhe.Sima Costantine Sima walishuka uwanjani na kuwapongeza Pamba Jiji FC kwa ushindi huo.
Wana TP Lindanda msimu huu wakiwa na mchanganyiko mzuri wa wachezaji waliotamba Ligi kuu msimu uliopita,mchezo wa fungua dimba uliopigwa uwanja wa Nyamagana waliichakaza timu ya Cosmo Politan kutoka Da- re-Salaam kwa mabao 4-0 kabla ya leo kuwafunga Pan African bao 1-0
Baada ya michezo hiyo miwili ya nyumbani ya Ligi ya Championship,Pamba Jiji FC sasa mchezo ujao watasafiri hadi Shinyanga kuumana na Stendi Utd Ijumaa ijayo kwenye dimba la Kambarage.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.