Tume ya Mipango ya Taifa leo tarehe 09 Oktoba, 2025 imewasili mkoani Mwanza kuendelea na kampeni yake ya kutoa mafunzo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali kuhamasisha ushiriki wa taasisi binafsi katika kufanikisha malengo ya muda mrefu ya maendeleo ya taifa.
Mafunzo hayo yamewakutanisha wadau mbalimbali wa sekta binafsi wakiwemo wawakilishi wa mashirika ya biashara, asasi za kiraia, taasisi za fedha, na wajasiriamali, ambao kwa pamoja wamepata elimu juu ya vipaumbele vilivyowekwa katika dira hiyo mpya ya taifa inayolenga kulifikisha Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa juu na ustawi wa watu kufikia mwaka 2050.
Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 imejengwa juu ya nguzo kuu tatu ambazo ni maendeleo ya watu, maendeleo ya uchumi, na utunzaji wa mazingira, ikiwa na dhamira ya kujenga taifa lenye mshikamano, haki, usawa wa kijinsia na ushiriki wa vijana katika maendeleo ya Taifa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.