TUMEJIPANGA KULINDA NA KUBAINI UDANGANYIFU WOTE WA MAZAO YA MAJINI: MKURUGENZI UVUVI
Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Mohamed Sheikh leo Machi 5, 2024 amefanya mazungumzo na mwenyeji wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Balandya Elikana na kusisitiza kwa kutambua uchumi wa ziwa Victoria Idara yake imejipanga kuhakikisha sekta hiyo inakuwa na mazingira rafiki kwa mvuvi.
Katika mazungumzo hayo mafupi mkurugenzi huyo amebainisha bado sekta hiyo haichangii mapato ya kuridhisha kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo uvuvi hatamu na udanganyifu wa baadhi ya wafanyabiashara.
"Tumepanga kuanza doria ziwani kuna utoroshaji mwingi wa mazao ya majini, na shughuli nyingine zote zinazofanywa kinyume na utaratibu tutazidhibiti cha msingi tupate ushirikiano mzuri", amesisitiza Mkuu huyo wa idara katika mazungumzo na mwenyeji wake.
Kwa upande wake Balandya amesema wataalamu wa uvuvi kutoka Ofisi ya mkuu wa mkoa wanaendelea kusimamia na kuzifanyia kazi changamoto zote Katika eneo hilo.
"Wataalamu wa uvuvi wamekuwa katika zoezi la kukagua mialo yote teule ya mkoa huu baadaye wataleta taarifa kwenu kwa hatua zaidi",Katibu Tawala wa mkoa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.