TUMIENI KEMIKALI KWA USAHIHI KUEPUSHA KUPOTEZA NGUVU KAZI YA TAIFA: RAS BALANDYA
Wasimamizi shughuli za usimamizi wa Kemikali wametakiwa kuzingatia muongozo uliopo ili kuepuka kupoteza nguvu kazi ya Taifa na uharibifu wa mazingira.
Rai hiyo imetolewa leo Novemba 19, 2024 na Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ndugu Balandya Elikana kwenye ukumbi wa mikutano TMDA, Buzuruga uliopo wilayani Ilemela wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kuhusiana na matumizi sahihi ya kemikali yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Kanda, amebainisha matumizi tofauti madhara yake ni makubwa kwa jamii na sehemu nyingine.
"Pamoja na faida nyingi za kemikali katika maisha ya kila siku ya mwanadamu,matumizi tofauti madhara yake ni makubwa kwa afya na mazingira iwe katika uzalishaji,usafirishaji na uhifadhi,"Katibu Tawala
Amewataka washiriki hao kuongeza umakini kwa muda wa siku mbili wa mafunzo hayo ili kutimiza malengo ya Serikali ya usalama muda wote wakati wa matumizi ya kemikali.
Aidha ameipongeza Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kutoa mafunzo hayo ambayo yataleta mageuzi chanya katika matumizi ya kemikali
Kwa upande wake Meneja Kanda kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Bw.John Mwanjala amesema awali kabla ya kutungwa sheria ya usimamizi na udhibiti wa kemikali za viwandani na majumbani ya mwaka 2003,kulikuwa na matumizi holela pamoja na uingizwaji nchini na kutumika pasipo usimamizi na kusababisha matukio mengi yaliyotokana na matumizi mabaya.
Washiriki hao wanatokea makundi mbalimbali ikiwemo kwenye migodi,viwanda vinavyozalisha vinywaji baridi na pombe pamoja na viwanda vya dawa mbalimbali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.