*Tumieni Taaluma yenu ya uhasibu na ununuzi ili muwe wasimamizi bora wa fedha za umma: RAS Balandya*
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ndg.Balandya Elikana ametoa rai kwa wahitimu wa Taasisi ya Uhasibu tawi la Mwanza (TIA) kuitumia vyema elimu yao ili kuleta mageuzi chanya katika usimamizi wa fedha za umma hapa nchini.
Akizungumza leo Novemba 24, 2023 kwenye viwanja vya Taasisi hiyo eneo la Nyang'homango wilayani Misungwi wakati wa mahafali ya 21, Balandya amebainisha Bado kuna changamoto nyingi katika usimamiaji mzuri wa fedha za umma ikiwemo watumishi kukosa weledi na badala yake kuingiwa na tamaa na kujinufaisha binafsi.
"Nyie wote hapa ni mashahidi wa taarifa ya mara kwa mara ya mkaguzi na mdhibiti wa fedha za Serikali (CAG) inavyoonesha upotevu mkubwa wa fedha za umma, miradi kutokamilika na fedha husika kuliwa sasa hayo yote mnatakiwa mkayafanyie kazi mtakao pata ajira Serikalini," amesisitiza Mtendaji huyo wa Mkoa wakati akizungumza na wahitimu hao.
Ameipongeza pia Taasisi hiyo kwa kuwajengea uwezo mzuri wahitimu katika kukabiliana na changamoto ya ajira kwa kuwa wabunifu wa kujiajiri.
"Nimejionea hapa kwenye mabanda yenu baadhi ya kazi za kujiajiri ambazo mmefanya, hii ni hatua nzuri sana kwani mkitoka hapa hamtakaa vijiweni na badala yake mtachangamkia fursa mbalinbali za kujiingizia kipato," Balandya.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania TIA Prof. William Pallangyo ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wake Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha Taasisi hiyo kuwa na majengo yake baada ya kutumia ya kupangisha kwa muda mrefu tangu mwaka 2012.
"Mradi wa jengo letu umeghatimu Shs bilioni 7.8 ni la kisasa litakaloanza kutumika April mwakani," Prof. Pallangyo
"Ndugu mgeni rasmi Taasisi yetu hadi sasa Ina matawi sita na tupo mbioni kuongeza la Saba huko Zanzibar lengo letu likiwa ni kuwazaluaga wataalamu bora watakao kuwa chachu ya kukuza uchumi wetu."Amesema Wakili Said Musendo Mwenyekiti wa bodi.
Awali kabla ya mahafali hayo mgeni rasmi alizindua kozi nyingine tano kwenye Taasisi hiyo ikiwemo masoko na Rasilimali watu na uhasibu na stadi za biashara.
Jumla ya wahitimu 947 wametunukiwa vyeti kwa ngazi mbalimbali kuanzia cheti, shahada na astashahada ya elimu ya
Uhasibu na manunuzi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.