Tumieni vikao vya Mabaraza Kuzalisha Takwimu sahihi kwa faida ya Taifa: RAS Mwanza
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ndg. Elikana Balandya leo Disemba 20, 2023 amefungua kikao cha tano cha Baraza la sita la wafanyakazi wa ofisi ya Taifa ya Takwimu na kuwataka kutumia vizuri jukwaa hilo kuzalisha Takwimu bora itakayoleta Maendeleo kwa Taifa.
Akizungumza na wajumbe wa Baraza hilo kwenye ukumbi wa mikutano Rock City Mall,Balandya amebainisha baraza hilo lina wajibu wa kujenga uelewa wa pamoja wa masuala mbalimbali ya Taasisi na kuhimiza nidhamu kwa upana wake, yote hayo yakifanyika kwa ukamilifu Serikali itaweza kupanga mipango yake ya maendeleo itakayokuwa na tija kwa wananchi.
"Ndugu wajumbe NBS ina jukumu la msingi la kuhakikisha takwimu zinazozalishwa nchini kwa matumizi mbalimbali zinakuwa bora,hivyo baraza hili litasimama kuwa chombo cha kufanya tathmini majukumu mbalimbali yanavyotekelezwa kwa ufanisi,"amefafanua Mtendaji huyo wa Mkoa wakati anazungumza na wajumbe wa baraza hilo wanalokutana kwa siku mbili.
Amewapongeza makamisaa wa Sensa ya watu na makazi 2022,Mhe Anne Makinda kutoka Bara na Mhe.Balozi Mohamed Hamza wa Zanzibar kwa kusimamia vizuri zoezi la Sensa iliyofanyika mwaka 2022 ambayo ilikuwa bora.
"Tunamshukuru Rais wetu Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa mafanikio ya Sensa hiyo ambayo ilifanyika katika mazingira ya kisasa ambapo sasa tunawarudishia matokeo yake wananchi kwa kuwaelimisha mipango mbalimbali ya kimaendeleo,"Mhe.Anne Makinda,Kamisaa wa Sensa 2022
Mtakwimu Mkuu wa Serikali Bi.Albina Chuwa amebainisha Sensa ya watu na makazi 2022 ilikuwa ni miongoni mwa Sensa bora ulimwenguni kutokana na kuwa na miundombinu ya kisasa hali iliyoleta ufanisi wa kazi wakati wa zoezi hilo.
Awali kabla ya kwenda kufungua kikao hicho Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza,Ndg.Balandya Elikana mapema asubuhi aliupokea ugeni Ofisini kwake uliofika kujitambulisha na mazungumzo mafupi ukiongozwa na makamisaa wa Sensa ya watu na makazi 2022, Mhe.Anna Makinda wa Tanzania Bara na Mhe.Balozi Mohamed Hamza kutoka Zanzibar.
Katika mazungumzo hayo Balandya amesema hali ya usalama Mwanza ni shwari na mvua zinazoendelea kuonyesha hazijaleta madhara makubwa gkulinganisha na mikoa mingine zaidi ya mafuriko ya muda mfupi kwa waliojenga kwenye njia za asili za maji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.