TUMUENZI BWIRE KWA KUENDELEZA MICHEZO MWANZA: RC MTANDA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewaongoza waombolezaji kuaga mwili wa aliyekuwa mkurugenzi wa kituo cha michezo cha Alliance Sports Academy, Marehemu James Bwire na kuwakumbusha njia pekee ya kumuenzi ni kuyatenda kwa vitendo mema yote aliyotenda ikiwemo kuendeleza michezo.
Akizungumza leo Januari 31,2925 wakati wa kutoa salamu za rambirambi nyumbani kwa marehemu Nyakato-mahina wilayani Nyamagana,Mkuu huyo wa Mkoa amesema enzi za uhai wake marehemu ametoa mchango mkubwa wa kuendeleza michezo na taaluma ya elimu kupitia vituo vyake vya michezo na shule,hivyo juhudi hizo hazina budi kuendelezwa.
"Marehemu Bwire nimebahatika kumfahamu ni mtu aliyekuwa na msimamo katika kile alichokuamini,timu yake ya Alliance hata pale ilipoanza kuyumba hakukata tamaa zaidi ya kusimama kidete kuipigania,"Mtanda.
Mtanda ameendelea kubainisha maendeleo ya michezo hayaji kimiujiza bali yanahitaji moyo wa kujitoa,uvumilivu na upendo pia mfano ambao hauna budi kuigwa aliyotuwachia Bwire.
"Leo tumeona ushuhuda wa baadhi ya wanafunzi na wanamichezo waliosoma shule za Alliance ambao sasa wamekuwa na mchango mkubwa katika Taifa wakiwemo wachezaji Israel Mwenda,Athanas Mdamu, Mapinduzi Balama,"Mkuu wa Mkoa
Aidha Mhe.Mtanda ametoa pole kwa familia ya Bwire kwa kuondokewa kwa mpigo mpendwa wao na mama yake mzazi na kuwaahidi kuendelea kushirikiana nao katika raha na shida.
Wakati huo huo Mkuu huyo wa Mkoa mapema leo asubuhi ameshiriki katika ibada ya mazishi ya aliyekuwa mrakibu mwandamizi wa jeshi la Polisi mkoani Mwanza Dkt.Aloyce Kessy.
Akizungumza mara baada ya ibada ya mazishi iliyofanyika kwenye viwanja vya Polisi Mabatini,Mtanda amesema marehemu enzi za uhai wake alitumia muda wake mwingi kupambania afya za wananchi wakiwemo askari wenzake,na kuwaomba waendelee kumuombea apumzike kwa amani peponi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.