TUNAHITAJI BIDHAA ZITAKAZOINGIA KWENYE MASOKO YA KIKANDA NA YA NJE: RAS BALANDYA
Wajasiliamali Mkoa wa Mwanza wametakiwa kuyatumia mafunzo waliyopata ili kuwajengea uwezo wa kuzalisha bidhaa zitakazokidhi viwango vya kuyafikia masoko ya kikanda na yale ya Nje.
Rai hiyo imetolewa leo Mei 9, 2024 Jijini Mwanza na Katibu Tawala Msaidizi Viwanda, Biashara na Uwekezaji Patrick Karangwa kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wazalishaji ili kuyafikia masoko ya kikanda na ya nje.
“Nawapongeza GS1 kwa kuunga mkono kazi za Serikali ambazo zitafanyika katika halmashauri zote nchini na nawaomba walengwa ambao ni wajasiliamali, wazalishaji na wanaviwanda kushiriki kikamilifu ili kuchochea ukuaji wa viwanda nchini," Karangwa.
Naye, Mkurugenzi wa bodi ya GS1 Tanzania Fatuma Kange amesema asilimia 90 ya wazalishaji Tanzania wapo katika sekta zisizo rasmi na hivyo basi amewaomba wajasiliamali kujiunga na GS1 Tanzania ili kuweza kupata fursa na taarifa mbalimbali za masoko ya nje na kikanda.
Naye mtaalamu wa uzalishaji, uandaaji wa bidhaa, viwango na ubora wa bidhaa Hamis Sudi amewashauri wajasiliamali kuzalisha bidhaa ambazo zimepitishwa na Shirika la viwango nchini (TBS), amewataka wajasiriamali kutumia mfumo wa barcode kupata masoko yaliyosahihi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.