Katika kuboresha mapendekezo ya Watanzania na kuwapatia fursa sawa katika mambo mbalimbali hasa maswala ya kisheria, Wizara ya Katiba na Sheria ipo katika mchakato wa kuandaa katiba mpya.
Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Waziri wa Katiba na Sheria amesema wapo katika mchakato wa kuanza kuandaa katiba mpya na kamati ya kudumu ya bunge ya Utawala Katiba na Sheria ina majukumu makubwa ya kusimamia katiba hiyo.
"Wote tunajua watanzania wote wanahitaji katiba mpya kama maelekezo ya chama cha mapinduzi kupitia kamati kuu yalivyo bayana, kwa hiyo na sisi tutaanza huo mchakato katika mwaka huu wa fedha.
Dkt. Ndumbro amesema hayo leo machi 16 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza alipokuwa anazungumza na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria ilipotembelea ofisini hapo wakiwa katika ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa kituo jumuishi cha utoaji haki na mradi wa kituo cha pamoja cha taasisi za sheria.
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima amesema kila Halmashauri ya mkoa wa Mwanza imetunga Sheria ndogo kulingana na mahitaji.
" Mkoa umekuwa ukisimamia halmashauri zake na kuhakikisha kuwa zinatunga sheria ndogo zinazohusiana na masuala ya utawala na ukusanyaji wa mapato.
"Mabaraza ya kata ambayo yapo kisheria yameimarishwa kila kata na yanafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria, jukumu la mabaraza hayo ni kufanya usuluhisho wa migogoro inayojitokeza miongoni mwa wananchi ndani ya kata zao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.