Hospitali ya Uhuru imetoa msaada wa hadubini mbili ‘microscope’ zenye thamani ya Sh milioni 6 kwa Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza kutokana na uwepo wa mahitaji makubwa ya vifaa tiba hasa za uchunguzi.
Akikabidhi mashine hizo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uhuru, Dkt. Derrick Nyasebwa, Mkurugenzi wa Tiba na bingwa wa upasuaji, Dkt. Emmanuel Kanumba alisema kama taasisi imefikia hatua ya kuisaidia Wilaya ya Ukerewe kutokana na ombi lao.
Dkt. Kanumba alisema mazingira ya wilaya ya Ukerewe yalivyo inapaswa kusaidiwa katika sekta ya afya kwani bila wananchi wa kisiwa hicho kuwa na afya njema hakuna maendeleo yatakayopatikana.
“Taasisi ya Uhuru hosptali inashirikiana na serikali na wadau mbalimbali kuhakikisha suala la afya halibaki kuwa jukumu la watu fulani bali ni la wote hivyo tumetoa msaada wa microscope baada ya kubaini upungufu huo uliopo katika wilaya ya Ukerewe.
Mara zote tumekuwa tukishiriki katika vikao mbalimbali vya sekta ya afya lakini taarifa nyingi kutoka Ukerewe ni upungufu wa vitendea kazi, sasa tukaona ni heri tukasaidia hizi mashine na imani yetu masuala ya vipimo vya maradhi hayatakuwa na shida tena,”alisema Dkt. Kanumba.
Dkt. Kanumba alisema hivi karibuni Serikali imezindua kampeni ya uwajibikaji katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi iliyokuwa na kauli mbiu ya ‘Jiongeze Tuwavushe salama’ hivyo kama taasisi ya Uhuru imeshiriki vema kwa kutoa mashine hizo ambazo zitakwenda kupima maradhi ya wagonjwa watakaofika hospitalini kupata tiba.
Alisema wamekuwa na utaratibu wa kusaidi jamii pale inapohitajika ambapo aliongeza kwamba hata watoto yatima hutibiwa bure na wale wenye kipato duni hutibiwa kwa gharama nafuu.
Aliwataka jamii kutoogopa kwenda hospitali za binafsi kwani kwa kuogopa gharama bali huwa zinasikiliza maombi ya mgonjwa na kumtibu kwa gharama nafuu.
Akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Lucas Magembe, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole, alishukuru uongozi wa hospitali hiyo kuona umuhimu wa kuisaidia jamii.
Kipole alisema vifaa hivyo vitakwenda kuitumiaka kama ilivyokusudia na kuwataka watumishi ndani ya wilaya hiyo kuituna mashine hiyo ili iweze kuwasaidia wananchi wengi.
Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella aliwasainisha kiapo cha uwajibikaji wakuu wa wilaya zote za mkoa huo juu ya kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga ambapo aliwataka kila mmoja awajibike katika eneo lake na kutoa taarifa ya utekelezaji kila baada ya miezi mitatu.
Tukio hilo lilifanyika wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uwajibikaji katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi iliyokuwa na kauli mbiu ya ‘Jiongeze Tuwavushe salama’ ambapo Mhe.Mongella alisema takwimu zinaonyesha kwamba mwaka 2017 jumla ya wanawake 195 walipoteza maisha kutokana na uzazi huo.
Mongella alisema kutokana na jitihada za Serikali za kupunguza haali hiyo, mwaka 2018 vifo hivyo vimepungua na kufikia 151 lakini kuanzia Januari mwaka huu tayari vifo 46 vitokanavyo na uzazi vimetokea ndani ya mkoa huo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.