USAJILI WA ALAMA ZA VIDOLE KWA WAGONJWA KWA KUTUMIA TEHAMA UTABORESHA HUDUMA ZA AFYA-RC MAKALLA
*Asema usajili utarahisisha tiba na ufuatiliaji wa wagonjwa wa VVU
*Ahaidi Serikali kuiunga mkono Shirika la ICAP kwenye Sekta ya afya kwa ujumla.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.CPA Amos Makalla amelipongeza Shirika la ICAP kwa kutoa vifaa vya TEHEMA kwa ajili ya usajili wa alama ya vidole kwa wagonjwa wa VVU kwenye Halmshauri zote nane Mkoani humo.
Akizungumza kwa niaba yake leo kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakati wa kupokea vifaa hivyo,Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe.Amina Makilagi amesema awali kulikuwa na changamoto ya upotevu wa kumbukumbu na ugumu wa ufuatiliaji kwa wagonjwa wa VVU,lakini sasa huduma hiyo itakuwa na tija.
"Shirika la ICAP mmekuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma kwenye vituo vya afya na kwa jamii,hatua hii ya vifaa hivi vya TEHEMA sasa tunakwenda kuimarisha taratibu za usalama,kuboresha taratibu za Utawala na huduma kwa wagonjwa kwa ujumla,"Amina Makilagi,Mkuu wa Wilaya Nyamagana.
"Leo tunakabidhi vifaa hivi vya TEHAMA vyenye thamani ya zaidi ya Shs milioni 314,lengo letu sisi kama ICAP ni kuiunga mkono Serikali katika kuboresha huduma kwenye sekta ya afya hasa maeneo ya vijijini na kwa jamii kwa ujumla,"amesema Dr.John Kahemele,Kaimu Mkurugenzi mkazi nchini,ICAP.
Naye mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Mhe.Sixbeth Gichagu amebainisha uboreshji wa huduma za afya ni miongoni mwa Ilani ya CCM hivyo ni wajibu wao kuiunga mkono ICAP katika harakati zao za kuboresha huduma za afya.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.