Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe Mhandisi Robert Gabriel ameagiza Halmashauri ya Ilemela kuandaa mazingira yenye mvuto zaidi ya Uwekezaji maeneo Kayenze ili kukuza Uchumi wa Mkoa wa Mwanza.
Mhandisi Gabriel ametoa maagizo hayo wakati akikagua maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya Uwekezaji huo yakiwemo maeneo ya Ufukwe wa Ziwa Victoria zitakapojengwa Hotel za kisasa.
"Nimefika hapa na kujiridhidha pasipo shaka mipango mliyoweka ya Uwekezaji na hasa baada ya kutazama ramani husika,hili eneo litainua Uchumi wa Mkoa wetu hapa ni kuhimizana barabara na Miundo mbinu yote ikamilike mapema" amesisitiza Mkuu wa Mkoa.
Kamishna ya Ardhi Mkoa wa Mwanza Elia Kamihanda amesema Serikali imeupa Mkoa wa Mwanza Shilingi Bilioni mia tatu na milioni miatano kwa ajili ya ukamilishwaji wa maeneo hayo ikiwemo kuwalipa fidia wakazi 400.
Amesema tayari jumla ya viwanja 3500 vimeshapimwa yakiwemo maeneo yatayojengwa Viwanda vidogo vidogo na mashamba maalum ya kilimo cha kisasa ambapo Viwanda hivyo vitatumika kumsaidia Mkulima kuchakata mazao yake.
Mkoa wa Mwanza unapakana na Mbuga ya Serengeti ambapo eneo la Kayenze litakuwa sehemu mwafaka kwa Watalii kufikia Hotel zitakazojengwa eneo hilo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.