VIJANA 300 KUNAFAIKA NA AJIRA KUPITIA MIRADI YA HALMASHAURI-DC UKEREWE
Ujenzi wa vyumba 36 vya maduka ya kisasa yaliyokuwa hatua ya mwisho kukamilika mjini Ukerewe ni miongoni mwa miradi inayotarajia kuwapatia ajira vijana 300 wilayani humo.
Mradi wa ujenzi wa maduka hayo 36 unaotokana na mapato ya ndani ya halmashauri ya Ukerewe utaipatia pia mapato ya kodi ya shs milioni 22 kwa mwaka fedha ambazo zitaongeza miradi zaidi kwa wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe.Christopher Ngubiagai ametoa taarifa hiyo leo Septemba 17,2024 wakati wa ukaguzi wa miundombinu ya masoko wilayani humo ukiongozwa na Katibu Tawala wa mkoa wa Mwanza Balandya Elikana.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema mara baada ya ukamilishaji wa maduka hayo ambayo yatatoa fursa kwa vijana kufanya biashara na usambazaji wa bidhaa kwa ujumla,mpango utakaofuata ni kuongeza maduka mengine 40 ambazo fedha zake zitatoka Serikali kuu.
Katibu Tawala huyo ameelekeza kwa halmashauri hiyo kuhakikisha wanatoa kwanza kipaumbele kwa wale walioondolewa kupisha ujenzi huo wa maduka.
"Ni jambo zuri mnapofanya utekelezaji wa miradi mbalimbali kwa mapato yenu ya ndani kwa faida ya wananchi,zidisheni ubunifu zaidi wa miradi ili kujiongezea mapato ya kodi na kuinua uchumi wa Wilaya hii",Balandya.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.