VIJANA WATAKIWA KUTUMIA VETA KUPATA UJUZI KWA GHARAMA NAFUU NA KUJIAJIRI
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ametoa wito kwa wazazi nchini kupeleka vijana wao kupata elimu na mafunzo ya ufundi stadi katika vyuo vya VETA nchini ili wapate ujuzi kwa gharama nafuu na kuweza kujiajiri.
Mhe. Mtanda ametoa wito huo leo Februari 28, 2025 kwenye hafla ya kilele cha maadhimisho ya miaka 30 ya utoaji huduma kwa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) yaliyofanyika katika viwanja vya chuo cha Mwanza.
"Leo tumeona katika maonesho ya vijana wetu jinsi gani wamepata ujuzi wa kutosha kwa fani mbalimbali jambo ambalo litawasaidia kujiajiri tena wamepata kwa gharama nafuu sana, natoa wito kwa vijana kutokaa vijiweni kuja kupata ujuzi." Mhe. Mtanda.
Akizungumzia darasa la madereva waliopewa ujuzi wa kuendesha magari na pikipiki amewataka vijana kufika kwenye vituo, kampasi na vyuo vya VETA nchini kwani kwa gharama nafuu ili kupata ujuzi utakao wasaidia kunusuru jamii kwa kuzuia ajali zinazoepukika.
"Zoezi la upandaji wa miti liwe endelevu kwenye taasisi na hata kwenye nyumba zetu kwani mabadiliko ya hali ya hewa yanategemea sana uhifadhi wa mazingira ili kutunza unyevunyevu na kusaidia hata kupatikana kwa maji kama kisima kilichokarabatiwa na VETA chenye umri mrefu." Amesema Mkuu wa Mkoa.
Awali, Mkurugenzi wa VETA Kanda ya ziwa CPA. Janeth Nyoni amesema kwa kipindi cha miaka 30 chuo kimekua na kuongeza vyuo hadi 11 tofauti na 3 vilivyokuwepo awali na kwamba kwa mwaka 2025 kanda hiyo imedahili jumla ya wanafunzi 5000 katika fani za muda mrefu na mfupi.
"Katika kuadhimisha miaka 30 ya utoaji huduma tumefanya shughuli mbalimbali kama kutoa mafunzo ya udereva bila malipo, kupanda miti, wanafunzi kuchangia damu, kukarabati majengo kwenye haspitali pamoja na kisima cha maji kwa wananchi wa kata ya Buswelu wilayani Ilemela." CPA Nyoni.
Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA) ilianzishwa mwaka 1995 na sheria ya bunge namba 1 ya 1994 ambapo ina jumla ya vyuo 80 nchini na 11 vikiwa katika kanda ya Ziwa ambapo mwaka 2026 vitaongezeka 14 na kufanya jumla ya vyuo 25.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.