Jamii imetakiwa kuzingatia mafundisho ya dini na kuyafuata ili kuepukana na uvunjifu wa amani ndani ya familia unaosababisha watoto kukimbilia mtaani.
Hayo yamebainishwa leo na Askofu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania ( AICT), Dayosisi ya Mwanza, Philipo Mafuja wakati akizungumza na waandishi kuhusu migogoro ya kifamilia.
Alisema suala la usaliti ndani ya ndoa, kutokuwa na elimu ya ndoa, uchumi wa familia kuwa mdogo pamoja na wazazi kutojua wajibu wao vinachangia watoto kujiingiza kwenye mahusiano wakiwa na umri mdogo.
Aidha, matatizo hayo yanachangia watoto hao baadhi yao kupata ujauzito ama kukimbilia mtaani.
Alisema jukumu la wazazi ni kuwaandaa vijana wao na kujua misingi ya ndoa kabla ya kuingia pamoja na kuwafundisha uvumiluvu katika maisha na kutopenda utajiri wa haraka.
" Elimu ndiyo msingi wa yote hivyo tuwahimize watoto kuzingatia suala la elimu na waondokane na tamaa ya kupata mali mapema," Mafuja.
Aidha, aliwaomba viongozi wa dini wawe na mafundisho ya mambo ya ndoa na kuwapa masomo mbalimbali vijana ili kuwasadia kuepukana na matatizo yanayochangia uvunjifu wa amani.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.