Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella ameziagiza halmashauri zote mkoani humo kuhakikisha ifikapo Aprili mosi mwaka huu ziwe zimefikisha asilimia 75 ya malengo ya makusanyo waliyojiwekea mwaka 2019/2020.
Akizunguza katika kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa(RCC) Mhe. Mongella alisema Serikali ya awamu ya tano imeelekeza nguvu katika kujenga uwezo wa ndani wa ukusanyaji wa mapato.
"Bajeti ya miradi ya maendeleo kwenye ofisi ya mkoa ni kidogo sana ambapa gharama zaidi ya asilimia 99 zipo kwenye halmashauri na wilaya huko ndiko kuna shughuli zinaendelea" alisema Mhe.Mongella.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Emmanuel Tutuba alisema Serikali itatoa ushirikiano kwa halmashauri kuhakikisha zinafanikisha zoezi la ukusanyaji wa mapato.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Senyi Ngaga na Mkuu wa wilaya ya Magu Mhe.Dkt. Philemon Sengati wakaelezea mbinu watakazotumia katika kusimamia zoezi la ukusanyaji wa mapato kuwa watahakikisha wanasimamia ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mifumo iliyowekwa na Serikali na kudhibiti mianya yote ya udanganyifu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.