VYAMA VYA USHIRIKA SIMAMENI IMARA KUONDOA UMASIKINI NCHINI: RC MAKALLA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla ametoa wito kwa vyama vya Ushirika nchini kusimama imara katika shughuli zao ili kuondoa umasikini na kuongeza ajira.
Akizungumza kwa niaba yake katika kilele cha siku ya Ushirika kwenye viwanja vya Furahisha ambapo kitaifa imefanyika Mkoani Mwanza, Katibu Tawala wa Mkoa huo Balandya Elikana amesema bado lipo kundi la Watanzania linaloishi katika hali ya umasikini hivyo kwa kupitia kazi za vyama vya Ushirika watakuwa mkombozi wa kuondokana na hali hiyo.
"Kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kuna kundi la Watanzania la asilimia 12 wanaoishi katika hali ya umasikini, ni matumaini yangu mipango imara ikifanyika kundi hilo litaondokana na umasikini kwa kupatiwa mikopo au shughuli za kujikwamua kiuchumi", Balandya.
Amevipongeza vyama vya Ushirika kwa kupiga hatua wakianzia na mitaji midogo na kufikia mitaji mikubwa hadi Trilioni moja na kuwataka kuendelea kuheshimu kanuni na sheria zinazowaongoza.
"Ndugu mgeni rasmi vyama hivi vya Ushirika vimekuwa vikifanya vizuri na mipango iliyopo sasa tumejipanga kuwa bora zaidi kwa upande wa Tehema ili shughuli zao zisambae hadi vijijini",Dkt.Abdulmajid Nsekeka,Mwenyekiti wa Tume ya kamisheni ya Ushirika Tanzania.
Akizungumzia hali ya vyama vya Ushirika nchini Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya vyama vya Ushirika Dkt.Benson Ndiege amebainisha hadi sasa wana mali yenye thamani ya Shs Trilioni 1.22 huku wakitoa mikopo ya Shs Trilioni 1.05
Katika kilele hicho cha ufungaji wa siku ya Ushirika,baadhi ya vyama vya Ushirika vilipatiwa tuzo mbalimbali kutokana na kufanya vizuri katka shughuli zao.
Kauli mbiu ya siku ya Ushirika mwaka huu inasema "Wanachama kusaidiana"
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.