Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.Adam Malima amesema waajiri wasiozingatia sheria za kazi watawajibishwa kwa kuchukuliwa hatua stahiki za sheria.
Pia amewataka waajiriwa (watumishi )kufanya kazi kwa kuzingatia misingi ya uwajibikaji na uwadilifu.
Mhe.Malima ameyasema hayo leo Mei Mosi, 2023 wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi yaliyofanyika kimkoa Wilayani Sengerema mkoani humo .
" Maagizo yangu kwa waajiri zingatieni sheria za kazi ikiwemo kuwasilisha michango ya wafanyakazi kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwa wakati,"amesema Mhe.Malima.
Mhe.Malima ameongeza kuwa katika kujali maslahi ya watumishi Serikali ya Awamu ya Sita,mkoani Mwanza imewalipa sh.bilioni 1.74 watumishi 571 walioghushi vyeti na sh.milioni 660 walilipwa watumishi 503 za malimbikizo yasiyo ya mishahara.
"Kazi inayofanywa na Rais Mhe.Dk.Samia Suluhu Hassan, ni kubwa,yapo maeneo itaendelea kujipanga kuboresha maslahi ya wafanyakazi na kufanyia kazi nyumba za watumishi na stahiki zingine hatua kwa hatua," amesema Mhe.Malima.
Awali Mratibu wa Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) mkoa wa Mwanza, Zebedayo Athuman, alisema baadhi ya waajiri wanakiuka sheria,hawawasilishi michango ya watumishi kwenye
mifuko ya jamii,hawatoi mikataba ya ajira na hawalipi mishahara kwa wakati.
."TUCTA tunaiomba Serikali ifanyie kazi changamoto hizo ili kuwapa nafuu wafanyakazi na kukomesha tabia za waajiri wasiozingatia sheria za nchi, " alisema Athuman.
Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi mwaka huu 2023 yameongozwa na kauli mbiu isemayo 'Mishahara Bora na Ajira za Stara ni Nguzo ya Maendeleo ya Wafanyakazi." Wakati ni sasa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.