Wabunifu wa TEHAMA kutatua changamoto mbalimbali Mkoa wa Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella amefungua kikao cha wabunifu wa Tehama katika kutatua baadhi ya changamoto zinazoukabili Mkoa wa Mwanza kilichofanyika katika Ukumbi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ikiwa ni juhudi zake za kukuza ubunifu na kukabiliana na changamoto mbalimbali nchini, ambapo kikao hicho kimefadhiliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi(COSTECH) kwa kushirikiana na (Atamizi) DTBi, ikiwa ni mwendelezo wa mpango wa kuibua vipaji vya ubunifu katika Tehama kwa kutumia vijana wabunifu kutoka Mkoa wa Mwanza.
Kikao hicho kimewapa fursa vijana waliochaguliwa kutatua changamoto mbalimbali za Mkoa wa Mwanza, kuwasilisha mada zao ambazo zina lengo la kutoa suluhisho la changamoto mbalimbali kwa kutumia matumizi ya Tehama, ambapo kimehudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka sekta za umma, sekta binfsi ( wavuzi, wakulima, wafanyabiashara) CTI, TCCIA, vyombo vya ulinzi na usalama, wataalamu kutotka ngazi ya Mkoa na Halmashauri za Ilemela na Nyamagama.
Suala la usalama ziwani lilichangiwa na wadau wengi kwani asilimia kubwa ya aeneo yanayozunguka ziwa Victoria ni wavuvi hivyo basi, mada iliwasilishwa kwa wadau na kugundua kuwa kuna changamoto mbalimbali zinazowakabili wavuvi na tatizo kubwa ni uvuvi haramu ndani ya ziwa Victoria unahatarisha mazalia ya samaki, pia uhalifu huu huandamana na suala la usalama wa vyombo vya usafiri ndani ya ziwa kwani mara kwa mara wavuvi wamekuwa wanaibiwa injini za vyombo vyao na kunyang’anywa samaki.
Baada ya kubaini changamoto hizo wataalamu wamekuja na mfumo ambao ni suluhisho la changamoto hizo kwa wavuvi na kwa sasa uko katika hatua za majiribio mara tu utakapokamilika utatumika kutatua shida za wavuvi za kiusalama na hivyo kupunguza na kudhibiti uvuvi haramu na uharamia ziwani.
Mfumo wa kukabiriana na changamoto za foleni za magari barabarani umeshatengenezwa, uko katika hatua za awali za majaribio, inatarajiwa kuwa jeshi la pilisi litatumia mfumo huu utakaobaini magari yasiyofuata sheria barabarani, kubaini ajari barabarani,kwa kuwa kutokana ka kukua kwa Jiji la Mwanza,msongamano wa watu na magari umeongezeka hivyo mfumo huu utatatua tatizo hilo, kwani watumiaji wataweza kupata taarifa ya barabara zenye msongamono mkubwa na hivyo kutafuta njia mbadala, hii itapatikana kwa kutumia simu za mikononi kwa wale watakaokuwa wamejisajiri kwa mfumo huu.
Mkoa wa Mwanza ni miongoni mwa mikoa yenye fursa nyingi katika maeneo ya ufugaji samaki, kuku na kilimo cha mboga mboga na matunda, ubora wa mazao kwa wazalishaji bado uko chini jambo linalowafanya wazalishaji kutokupata masoko ya uhakika yanayowawezesha kukuza kipato chao, hivyo mfumo umeundwa utakaobaini changamto zilizopo katika jiji la Mwanza, na utasaidia wajasiriamali katika maeneo mbali mbali kupata elimu na majibu ya changamoto zinawakabili hasa katika ufugaji wa samaki, kilimo cha mboga mboga, matunda na ufugaji wa kuku wa kisasa na kienyenyeji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.