Wachezaji kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza waagwa kushiriki SHIMIWI Iringa
Afisa Elimu Mkoa wa Mwanza Martin Nkwabi amewataka Wachezaji kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo wanaokwenda kushiriki Michuano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) mkoani Iringa kwenda kucheza kwa bidii ili warudi na ushindi.
Ndugu Nkwabi ametoa wito huo leo Septemba 26, 2023 wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wachezaji hao iliyofanyika kwenye Ofisi za Elimu ambapo ufunguzi rasmi wa michuano hiyo unatarajiwa kufanywa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Oktoba 04, 2023.
Akizungumza na timu hiyo yenye jumla ya wachezaji 15 watakaokipiga kwenye michezo ya Mpira wa Pete, Karata, Riadha, Baiskeli, Drafti na Kurusha Mishale Nkwabi amewataka kwenda kuzingatia walichofundishwa kwenye mazoezi na kuhakikisha wanarudi na vikombe vya ushindi.
"Ushindani unaleta maendeleo, ni lazima twende na ari ya ushindi tuone furaha ya kurudi na ushindi na katika kufanikisha hilo ni lazima twende na moyo wa ushindani na ushirikiano wa pamoja ili tufanikiwe lengo letu." Nkwabi amesisitiza.
Kaulimbiu ya Michuano hiyo (SHIMIWI) mwaka huu inasema "Michezo mahala pa kazi huimrisha afya na kuongeza ufanisi kazini".
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.