MKUU wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella amepokea vifaa kutoka kwa wadau mbalimbali ikiwa ni sehemu yao ya kushiriki katika mapambano ya kukabiliana, kujikinga na homa kali ya mapafu inayosababishwa na kirusi aina ya Covid-19 .
Mongela akizungumza baada ya kupokea msaada huo kutoka Plan International, Railway Children ,TBL pamoja na kampuni ya Kiboko anasema anawashukuru kwa kujitoa kwao kwa kuwa misaada yote itaelekezwa kwenye jamii, watoa huduma na kwa wale waliopo kwenye huduma za tiba.
Anaongeza kuwa ushirikianao unahitajika ili kuwakomboa wananchi na janga hilo na kuomba wadau wengine wajitokeze ili kuiunga mkono serikali na kuokoa maisha ya watanzania huku akiwataka wananchi wote kuzingatia maelekezo ,kanuni zinazotolewa na Wizara ya afya sambamba na kuzingatia ufanyaji wa mazoezi.
Akizungumza wakati akitoa msaaada huo Meneja wa kitengo kutoka plan International Tanzania Dr Majani Rwambali anasema vifaa walivyokabidhi ni vifungashio elfu 12000 venye ujanzo tofauti na barakoa 4166 vyote vikiwa na thamani ya 16,858,000 hivyo wanaendelea kutoa michango yao ili kuisaidia serikali katika maeneo mbalimbali wanapotekeleza miradi yao kama Rukwa,Geita, Kigoma, Mwanza,Pwani,Dodoma,Morogoro pamoja na Dar es Salaam.
Kwa upande wake Meneja mradi shirika la Railway Children Africa Abdalah Issa anasema wametoa magodoro, sabuni na vitakasa mikono ili kuungana na serikali katika mapambano yake ya kuutokomeza ugonjwa huo ambao umeenea nchini na wanatarajia kuendelea kutoa mchango zaidi kwa mkoa na Halmashauri zote zilizopo mkoani humo.
Huku Mkuu wa kiwanda cha TBL Patel Kilovele akieleza sababu za kutoa lita 500 za vitakasa mikono anasema wanaguswa na maisha ya watanzania hivyo msaada huo utasaidia kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo pia alitoa ahadi kwa serikali kampuni yao itaendelea kushirikiana na serikali katika vita na jitihada zakutokomeza ugonjwa huo.
Naye ofisa masoko kutoka Kiboko Paints Atul Mukhraiya akisema Corona na ugonjwa hatari ambao unasamba kwa kasi hivyo wao wamewiwa kutoa matenki madogo 25 kwa ajili ya kutunzia maji ya kunawia pamoja na mabeseni vifaa hivyo vitasaidia wananchi katika maeneo mbalimbali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.