Wafanyabiashara wadogo wadogo wa karanga,viungo na miwa ya kufunga wameishukuru serikali kwa kuruhusu vifungashio vya plastiki vitumike kufungia bidhaa zao.
Awali wafanyabiashara hao walijawa hofu na kuamua kuamishia bidhaa zao kwenye ndoo zinazoonesha wakiofia kuziweka kwenye vifungashio ambavyo ni vya plastiki.
Hata hivyo, hofu yao iliisha baada ya Afisa Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Mazingira (Nemc), Abel Sembeka kusema kuwa vifungashio vinavotumika kufungia bidhaa zao vitaendelea kutumika ili mradi viwe na nembo ya Shirika la Viwango Tanzania, TBS.
“Kuna watu wanawasiwasi juu ya mifuko ya kufungia karanga,miwa,viongo vya pilau na kadharika, vifungashio hivyo havijakatwaza, vitumike lakini baada ya kudhibitishwa na tbs”alisema Sembeka
Riziki Thomas mfanyabiashara wa bisi(popcorn)alisema”Tunaishukuri serikali kwa kutythamini wajasiliamali wadogo kwa kuturuhusu kutumia vifungashio vya plastiki kufungia biashara zetu”
Akizundua rasmi matumizi ya mifuko mbadala na marufuku ya mifuko ya plastiki, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh John Mongella aliwataka wakazi wa mkoa huo kuvumilia bei zilizopo sasa za mifuko hiyo kuwa zitashuka baada ya siku kadhaa kutokana na wafanyabiashara kuanza kuingiza mifuko hiyo mkoani humo.
“Hakuna jambo jipya lililowahi kutokea binadamu asipate mshituko, kutoka na katazo hili, vijana na kina mama mtumie vizuri hii fursa kwa kutengeneza mifuko ya makaratasi” alisema Mongella.
Alisema, kwa mtu yeyote atakaye kutwa na mfuko wa plastiki atauonesha uongozi wa mkoa mahali alipoutolea huku hatua zingine za kisheria zikifuata.
Naye Naibu Meya wa jiji la Mwanza Biku Kotecha alitaka wananchi wasisumbuliwe kwa kupigwa au kuombwa rushwa wakati wa zoezi la kuhakikisha hakuna matumizi ya mifuko hiyo jijini humo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.