Balozi wa Namibia nchini, Mheshimiwa Theresia Samaria ameahidi kuwaleta wafanyabiashara kutoka Namibia ili kuangalia fursa za biashara hasa katika sekta ya samaki na ngozi.
Akiwa na mwenyeji wake, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella, Balozi huyo amesema kwamba hakutarajia kuona fursa za kibiashara zilizopo mkoani Mwanza.
“Biashara ya samaki inafanana na kwetu, labda tofauti ni aina ya samaki. Sikutarajia kuona hali hii na fursa zilizopo kwa wafabiashara wa Namibia”, alisema akitolea mfano wa ukame ulioikumba nchi hiyo kwa miaka mitano mfululizo na kusababisha uhaba wa vyakula vya mifugo, “tulienda kila mahali kutafuta chakula cha mifugo, hatukufikiria kabisa Tanzania”.
Balozi Theresia na mwenyeji wake Mongella walitembelea viwanda vya kuchakata samaki vya Omega Fish Ltd na Tanzania, Kiwanda cha Ngozi cha Africa Tanneries Limited pamoja na Soko la Kimataifa la Samaki la Kirumba jijini Mwanza.
Kuhusu kiwanda cha ngozi, Balozi Theresia alisema amewasiliana na mmoja wa viongozi katika taasisi inayohusika na usindikaki wa ngozi ili atembelee kiwanda hicho, “Tanzania ipo nafasi ya saba kwa idadi ya ng’ombe Afrika, nimeangalia kiwanda na nimewasiliana na Kaimu Mwenyekiti aje Mwanza”.
Kiwanda cha Africa Tannaries kilibinafsishwa miaka kadhaa iliyopita, lakini serikali ilikichukua tena baada ya mwekezaji kushindwa kuendelea na uzalizashi.
Naye Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa Mongella amewahimiza wafanyabiashara jijini kuwa wapambanaji katika kupigania fursa zilizopo.
“Tuwe wapambanaji zaidi nguvu ya soko hazitaki watu laini laini.
Sekta binafsi inazidi kuimarika na kushamili serikali pia inapata nafasi zaidi ya kutoa huduma za kijamii kwa sababu inapata kodi na tozo mbalimbali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.