WAFAYABIASHARA WA DAWA WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ILI KUEPUKA KUMDHURU MWANANCHI: RC MTANDA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewataka wafanyabiashara wa dawa kuepuka aina yoyote ya udanganyifu na badala yake wafuate Sheria na kanuni kutoka Mamlaka ya dawa na vifaa tiba TMDA.
Akizungumza leo Mei 17, 2024 eneo la Magereza, Butimba wakati wa hafla fupi ya kuwakabidhi msaada wa dawa kwa Jeshi hilo zilizotolewa na Mamlaka ya dawa na vifaa tiba (TMDA), Mtanda amesema bado wapo baadhi ya wafanyabiashara wanaofanya udanganyifu wa magendo na kuuza dawa zisizo sahihi hali ambayo inakuja kumdhuru mwananchi.
"TMDA nawapongeza kwa kuendelea kuonesha kuijali Jamii kwa kutoa msaada huu wa dawa zenye thamani ya shs milioni 56.4 kwa ajili ya Zahanati za Magereza,rai yangu kwenu kupitia wakaguzi wenu ongezeni bidii kuwabaini wale wote wanaofanya shughuli hii kinyume na utaratibu na wafikishwe kwenye vyombo vya kisheria,"Mkuu wa Mkoa
Aidha Mhe.Mtanda amezitaka Taasisi nyingine kuiga mfano wa TMDA wa kujali kuhudumia Jamii kwani kwa kufanya hivyo tunazidi kujenga jamii inayoishi kwa upendo na ushirikiano
Meneja wa Mamlaka ya dawa na vifaa tiba Kanda ya ziwa Mashariki,Sophia Mziray amebainisha huo ni utaratibu wao wa kila mwaka ambapo mwaka jana walitoa msaada wa dawa hizo wenye thamani ya shs milioni 58.
"Tunashukuru sana Taasisi hii kwa kuendelea kutujali,kama mjuavyo Jeshi letu lina shughulika na wafungwa na wanahitaji pia matibabu wanapokuwa wanatumikia vifungo vyao,msaada huu umelenga mahali mwafaka kabisa",Justin Kaziulaya,Mkuu wa Magereza,Mwanza.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.