WAFUGAJI MISUNGWI WATAKIWA KULILINDA SHAMBA LA MIFUGO MABUKI
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameuagiza uongozi wa Wilaya ya Misungwi kushirikiana na shamba la mifugo la Mabuki kudhibiti wafugaji wanaoingiza mifugo yao katika shamba la Serikali na kuliharibu.
Mhe. Mtanda ametoa agizo hilo leo tarehe 13 Januari, 2025 alipofanya ziara kwenye shamba hilo lililopo wilayani Misungwi ambalo limeanzishwa mwaka 1967 na Serikali kwa madhumuni ya kuzalisha mbegu bora za madume (Mitamba).
RC Mtanda amesema, wananchi wana wajibu wa kuenzi juhudi za baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambaye alianzisha shamba hilo lenye hekta 9763 na kwamba alipeleka ng'ombe wawili wa kisasa kwa ajili ya kuanza uzalishaji ambao uzalishaji umeendelea kwa dahari ya miaka.
Aidha, ametoa wito kwa Wizara ya mifugo kuendelea kuwajengea uwezo vijana wengi zaidi kupitia programu ya Jenga Kesho Bora (BBT) kwa kuwapatia mafunzo ya ufugaji shambani hapo kama ambavyo vijana 1200 walipelekwa na kuhitimu wakiwa wafugaji bora.
Naye Meneja wa Shamba hilo Bi. Lini Mwala ametaja changamoto ya wafugaji kuingiza mifugo kwenye shamba hilo na kubaribu malengo ya uanzishwaji wake ambapo wanashirikiana na taasisi za TARIRI wanatafiti na kutoa elimu ya ufugaji wa kisasa pamoja na LITA wanaoendesha mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa vijana.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.