WAFUGAJI WA KUKU KANDA YA ZIWA WAKUMBUSHWA KUCHANGAMKIA FURSA ZINAZOTOLEWA NA SERIKALI
Wafugaji wa kuku kanda ya ziwa wamekumbushwa kuichangamkia fursa zinazotolewa na Serikali ikiwemo mikopo na mafunzo ili kujiimarisha kiuchumi.
Rai hiyo imetolewa leo Mei 3, 2024 na Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Emil Kasagara kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa umoja wa wajasiriamali wa wafugaji kanda ya ziwa (UWAU) kwenye ukumbi wa Nyakahoja na kuwataka wapige hatua na wenye tija kutokana na soko zuri la kuku hivi sasa
"Serikali ya awamu ya sita imezidi kutoa kipaumbele katika shughuli za uzalishaji ikiwemo kilimo,mifugo na uvuvi kwa kutoa fedha nyingi,hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha mnazidi kuwa wazalishaji bora na imara kwa kuichangamkia fursa hizo,"Kasagara
Amewashukuru wataalam wa mifugo Lina Feeds kwa kuwajengea uwezo wajasiriamali hao kwa lengo la kuwa wazalishaji wazuri.
"Mkoa wetu una fursa nyingi ikiwemo migodi,tunapokuwa na uzalishaji bora wa kuku na mayai tutaweza kupata soko la uhakika kwenye maeneo hayo,hivyo rai yangu kwenu mzingatie vizuri mafunzo haya," amesisitiza Katibu Tawala Msaidizi
Mwenyekiti wa UWAU Bw.Madaraka Mchunguzi amebainisha wafugaji wengi bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mitaji, mifugo kufa,ukosefu wa masoko na mbinu za ufugaji wenye tija,sasa wana imani ya kuja na matokeo chanya baada ya kupata mafunzo hayo
"Napenda kuwashukuru wawezeshaji hawa kwa kutupatia elimu hii,mifugo yetu ilikuwa inakufa sana na kushuka kwa uzalishaji wetu,tunaomba kupatiwa mafunzo haya mara kwa mara,"David Kitundu,mfugaji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.