Wakaguzi wa ndani wa Halmashauri wametakiwa kuangalia viashiria hatarishi katika miradi ambayo serikali imetoa fedha za utekelezaji ili kunusuru upotevu wa mapato.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel wakati wa kikao cha miradi ya ujenzi wa vituo vya afya, ujenzi wa vyumba vya madarasa na kusaini mkataba wa nyongeza wa utekelezaji wa mkataba wa lishe.
Amesema haipendezi miradi kuharibika alfu wakatafutana hivyo waanze vizuri kwa kuweka mifumo ya udhibiti na kushauriana ili miradi iende vizuri.
Amesema alizunguka Halmashauri zote na kubaini wakaguzi walikuwa na tatizo la kutokagua miradi yote ambayo inatekelezwa ikiwemo ya serikali kuu.
Hivyo amewaagiza wakurugenzi kuhakikisha kwenye mpango wao wa kutumia fedha bila kujihakikishia usalama wake ni hatari hivyo wahakikishia mkaguzi wa ndani anatamiza jukumu lake la kimsingi kwenye kukagua miradi yote.
Amesema kuna tatizo kubwa la miundombinu katika miradi ya afya na elimu hivyo fedha zinatakiwa za kutosha sambamba na usimamizi ili kupiga hatua pamoja kuweka nguvu kwenye ukusanyaji wa mapato .
Aidha akizungumzia suala la lishe baada ya kusaini mkataba wa utekelezaji amesisitiza matumizi ya lishe kwa wananchi ili kujenga Taifa lenye afya, kujijenga kiuchumi na kuepukana na magonjwa mbalimbali ambapo kila mmoja anahitaji lishe ili kuwa na afya bora.
Amesema wamesaini mkataba kwa ajili ya lishe hivyo isiwepo Halmashauri ambayo haitotoa mchango wake kwa mujibu wa bajeti na maelekezo kwa ajili kuhakikisha suala la lishe linatekelezwa .
" Usikute nao wanaotekeleza huu mpango ndani ya jiji wanachangamoto ya lishe kwa sababu vionja vya tatizo la ukosefu wa lishe ni kushindwa kufikili na kufanya maamuzi kwa sababu lishe bora inazuia kufanya maamuzi tukiwa na watendaji wengi wanaoshindwa kuelewa vitu kwa uharaka shida hapo ni lishe" anaeleza Mkuu wa Mkoa.
Mwisho.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.