Katika kuadhimisha sikukuu ya wakulima maarufu kama Nane Nane leo tarehe 2 agosti 2025 Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bw. Balandya Elikana ametembelea mabanda mbalimbali katika viwanja vya maonesho ya Nane Nane Nyamhongolo jijini Mwanza.
Akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa serikali na wataalamu wa kilimo Balandya alipata fursa ya kujionea teknolojia mpya ubunifu wa vijana katika kilimo na bidhaa mbalimbali zinazozalishwa kwa kushirikiana na taasisi ya kilimo (TARI).
Akizungumza katika banda la Tari na wakulima waliokusanyika Balandya aliwapongeza wakulima kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuhakikisha Taifa linajitosheleza kwa chakula.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa kutumia mbinu bora za kisasa ili kuongeza tija shambani na hatimaye kuongeza mavuno ya mazao yao.
“Sikukuu ya nane nane si tu kusherehekea mafanikio ya wakulima wetu, bali ni jukwaa muhimu la kujifunza kubadilishana maarifa na kuhamasishana kuhusu umuhimu wa kilimo endelevu, tuendelee kuwekeza katika teknolojiai.” Amesisitiza.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.