Wakurugenzi wa Halmashauri na maofisa mbalimbali wa wateule wameapishwa mkoani Mwanza kwa ajili ya mchakato wa kusimamia uchaguzi wa Serikali za mitaa huku wakionywa kwamba atakayekiuka kiapo ataadhibiwa kwa sheria ya usalama wa taifa.
Akizungumza na wakurugenzi hao kabla ya kuwaapisha, Hakimu kutoka Mahakama ya Mkoa wa Mwanza, Bonaventure Lema, alisema yeyote alikayeapa na kutoa siri kwa mtu asiyehusika atachukuliwa hatua za kisheria kwa kutumikia jela zaidi ya miaka 20 kwa kutumia sheria ya kutunza siri ya usalama wa taifa hata akiwa amestaafu.
“Kazi yangu iliyonileta hapa ni ndogo tu ya kuwaapisha na kurudi katika eneo langu la kazi kuendelea na majukumu ya kila siku wala sihitaji kupata mafunzo yenu, baada ya kiapo hiki naomba kama wewe ni mfuasi wa chama chochote cha siasa tambua kiweke pembeni.
“Baada ya kukamilisha shughuli iliyosababisha ule kiapo ni ruksa kurudia chama chako na kuendelea na uanaharakati, naomba kila mmoja anieleze maana ya siri au nielezeni siri ya watu wawili ni siri,”alihoji huku wajumbe hao wakimjibu sio siri.
“Naomba niwaambie siri ni jambo lolote ambalo hupaswi kulisema kwa mtu mwingine, hiyo ndiyo siri sasa baada ya kuapa hapa hatutarijii tena mtu anakwenda kumwambia mtu mwingine kisha anamwambia hiyo ni siri, hatua zitachukulia na haijalishi kama umestaafu, sheria za kutunza siri ya usalama wa taifa zitachukua mafasi yake,”alisema.
Awali, akifungua simina ya mafunzo kwa wakurugenzi hao na maofisa wengine wateule, Kamishna wa Tume ya Uchaguzi nchini (NEC), Asina Omar aliwaonya mawakala wa vyama vya siasa kuingilia utendaji kazi ya watalaam badala yake wapaswa kuwapo katika vituo ili kushuhudia namna shughuli inavyofanyika kwa haki.
Omar alisema mawakala anaruhusiwa kuwapo katika maeneo ya vituo lakini si kwa ajili ya kufanya kazi ambayo hawana uzoefu wala mafunzo, hivyo wanapaswa kutambua wao wafanye kazi waliyoagizwa na vyama vyao kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa.
Kuhusu mafunzo kwa wakurugenzi na maofisa , alisema lengo ni kuwaongezea uelewa na matumizi ya ya mashine ya BVR kit itakayotumika katika kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura.
Alisema uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika Mkoa wa Mwanza linatarajiwa kufanyika kuanzia Agosti 13 hadi 19 ambapo aliwataka watumishi wote wakiwamo wakurugenzi, maofisa uchaguzi wa halmashauri na watalaamu wa Tehema kutimiza wajibu na majukumu yao ipasavyo na kutoa elimu kwa waandikishaji.
“Kila mmoja atimize wajibu wake na mnapaswa kuelewa hatutaki tena kufanya shughuli hii kwa mazoea, wapo wenye uzoefu na shughuli hii hawapaswi kupuuza kwa kigezo wanajua hapana, hakikisheni mnafuatilia hatua kwa hatua, toeni elimu pale unapona inahitajika.
“Mjiamini kama watu mliopewa mafunzo lakini kikubwa ni kuzingatia sheria na miongozo iliyowekwa, jaribuni kuonyesha kujitambua na kutambua miundombinu mtakayokwenda kufanyia kazi, wale wa tehema hakikisheni linapojitokeza suala linalowahusu tatueni haraka, kama lipo linahitaji sisi kuhusika tujulishane haraka,”alisema.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.