Wamachinga mkoa wa Mwanza wafanya maandamano ya kumpongeza Mhe.Rais Dkt.John Magufuli kwa mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu COVID -19 tangu uingie nchini na kutowaweka watanzania kwenye zuio la kutotoka nje (lockdown).
Kauli hiyo ilitolewa kwa nyakati tofauti na na machinga hao akiwemo Mwenyekiti na Makamu mwenyekiti wa Shirika la Umoja wa Machinga Jiji la Mwanza, Said Tembo na Joseph Mwita wakati wakizungumza na waandishi wa habari wanasema wanaobeza hatua ya Mhe. Rais kuwataka wananchi kuendelea kufanya kazi wapuuzwe.
Tembo alisema Machinga wanamuunga mkono Mhe. Rais Dkt. Magufuli kwa uamuzi wake mgumu na msimamo wa kutowaweka Watanzania kwenye zuio kwani alitambua umuhimu wa wananchi wake na kuwathamini .
Alisema kuwa Rais aliamini na kumtanguliza Mungu katika kupambana na corona kuliko binadamu wenyewe na kuna baadhi watu walitabiri Watanzania wengi watakufa kwa ugonjwa huo lakini hadi leo hata waliokuwa wameugua wamepona.
“Wapo wanaombeza Mhe.Rais Dkt.Magufuli kuwa hakufanya jambo la busara kutowaweka Watanzania kizuizini hatupingi na tunatambua ugonjwa huo upo na hata yeye juzi akiwa Chato kanisani alisema katika kupambana na ugonjwa huo kila mtu anatumia mbinu yake.Hivi ukikaa ndani siku nne tu biashara hii ya kuingiza na kutoa mguu ndio ule hali ingekuwaje,”alihoji mwenyekiti huyo wa Machinga.
Alieleza kuwa laiti ingetokea ikawekwa karantini hakuna mfanyabiashara mdogo au mwananchi wa kipato cha kawaida mwenye bajeti ya kumudu kuendesha maisha kwa mwezi mmoja hivyo watanzania wana kila sababu ya kumpongeza na kumuunga mkono Mhe. Rais, amewawezesha kuendelea kuchapa kazi.
Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa Shirika hilo la Machinga, Joseph Mwita anasema wanamshukuru Mhe. Rais Dkt. Magufuli kwa alichokifanya kwa kuwatoa hofu wafanyabiashara na watanzania kuwa hakuna mtu wakufungiwa ndani huku akiwataka waendelee kufanya kazi kwa kujiamini ingawa corona ipo.
“Ametoa takwimu za mambukizi ya ugonjwa huo,ameyakabidhi maisha ya wananchi na taifa kwa Mungu hivyo na sisi tumkabidhi kwa Mungu ampe maisha marefu huku tukichukua tahadhari na kufuata maelekezo ya serikali na wataalamu wa afya,”alisema Marwa.
Aidha, mjasiriamali katika Soko Kuu la Mwanza, Ester Mgaya alisema hawana budi kumshukuru Mungu lakini pia Rais kwa uamuzi wake mgumu wa kuwatoa hofu watanzania wasitishwe na corona yakuwa hali ikiendelea hivi ataruhusu vyuo vifunguliwe na kushauri kuendelea kumwomba Mungu ili corona itokomee.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.