WANAHABARI MWANZA WATAKIWA KUTOA HABARI SAHIHI KUELIMISHA JAMII
Waandishi wa Habari mkoani Mwanza wamekumbushwa kuzingatia maadili ya taaluma yao wakati wanatimiza majukumu ya kila siku ili jamii ijengwe kwenye misingi ya ukweli.
Rai hiyo imetolewa jana tarehe 13 desemba, 2024 na mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Christopher Ngubiagai kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwenye hafla ya usiku wa Wanahabari iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mwanza Hoteli.
Amebainisha vyombo vya habari ni muhimili muhimu hivyo ili kuepuka migongano isiyo na tija waandishi wa habari wana wajibu wa kujiridhisha na usahihi wa kile wanachokusudia kuwafahamisha wananchi.
"Ndugu zangu wana habari wote hapa ni mashuhuda Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan anavyozidi kuwawekea mazingira mazuri ya kazi zenu na hasa anavyosisitiza ushirikiano baina ya Serikali na vyombo vya habari, tuendelee kutumia kalamu zetu vizuri na hata pale kwenye kukosoa uungwana utumike na isiwe karaha kwa mlengwa,"mkuu wa wilaya.
Comrade Ngubiagai ametolea mfano Mkoa wa Mwanza umekuwa na miradi mingi ya kimkakati,waandishi wa habari wanatakiwa kutumia nafasi hiyo ili wananchi wapate ufahamu wa kina namna Serikali yao inavyowaletea maendeleo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha waandishi habari mkoani Mwanza,MPC Bw.Edwin Nsoko amesema huo ni utaratibu waliojiwekea wa kila mwaka kuwa na usiku wa pamoja kwa kushirikiana na wadau wao mbalimbali na kubadilishana uzoefu wa shughuli zao.
"Mheshimiwa mgeni rasmi kazi zetu zinahitaji ushirikiano wa dhati ili kutimiza vizuri majukumu yetu hapa zipo Taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi ambazo tumeshirikiano nazo kuhakikisha tunajenga uchumi wa Taifa letu,"Mwenyekiti MPC
"Hivi sasa tunazidi kujiimarisha katika sekta ya usafiri wa maji kwenye maziwa ya Victoria,Tanganyika na Nyasa,Meli mpya ya Mv Mwanza ipo mbioni kuanza safari zake na itafika hadi Kenya na Uganda,ni dhahiri shughuli za kiuchumi zitapiga hatua hivyo vyombo vya habari vina wajibu wa kuwaemisha wananchi fursa zilizopo kupitia mradi huu,"Erick Hamisi,mkurugenzi mtendaji TASHICO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.