Wananchi wa Wilaya ya Misungwi watakiwa kufanya maamuzi ya kweli kwa kumpigia kura kiongozi atakayewaletea maendeleo bila kujali tofauti za vyama .
Mjumbe wa kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa , Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi hao wakati akimuombea kura mgombea Urais wa CCM,Dk.John Magufuli na wagombea ubunge na udiwani wa chama hicho.
Alisema maendeleo hayana chama hivyo ni vyema wakamchangua kiongozi atakaye weza kuchapa kazi na kuleta maendeleo kwa watanzania wote wakimwemo wanyonge.
Alisema wametekeleza miradi mbalimbali ikiwemo,maji ambapo kwa Sasa wanateknolojia mpya ya kutoa maji ziwani,elimu, Ujenzi wa barabara ambapo wananchi watarajia mambo makubwa ambapo wamemaliza ujenzi kwa hatua za mikoa kwa sasa wameanza za wilaya pia wanaboresha njia zote za usafirishaji ili kukuza uchumi wa wananchi hao.
Pia aliwataka wananchi hao kuwapeleka shule watoto kwani sekta hiyo imeboreshwa kwa kiwango kikubwa pia mchakato wa kujenga mabweni kwenye shule za sekondari unaendelea.
Aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo Charles Kitwanga akizungumza na wananchi hao alisema serikali imefanya mambo mengi ikiwemo ujenzi wa hospitali mpya ambayo fedha zake zimeshaingizwa.
Pia alieleza kuwa barabara ,kutatuliwa kwa changamoto ya maji iliyokuwa ikiwakabili kwa muda mrefu Sasa yanatoka ambapo Billion 12 zilitolewa na Rais Magufuli za mradi wa maji Usagara.
Alisema mardi wa Usagara wamepokea billion 72 za kutoa maji chanzo Cha Butimba ambapo mkandarasi ameanza kazi itaendelea kufanyika ili kuondoa changamoto hiyo pia alitumia fursa hiyo kuwaomba samahani watu wote aliowakosea .
" Fedha za mradi huo wa maji usagara zimetoka mdogo wangu (Mnyeti) zisimamie hizo fedha zisije zikaenda kusikojulikana usimamie vyema usije ukafanya mambo yetu yale mengine kwa sababu CCM inasimamia maadili" alisema Kitwanga.
Nae Mbunge mtarajiwa wa Jimbo hilo Alexander Mnyeti alisema anachosubili ni kuapiswa ili kuwafanyia kazi wananchi hao na kuwaletea maendeleo na siyo maneno kwani uwezo ,nguvu zote zipo hivyo wanachopaswa ni kumpigia kura mgombea Urais John Magufuli.
Pia aliongeza kuwa ujenzi wa barabara utafungua uchumi wa Misungwi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.