WANAWAKE USHIRIKA MWANZA WAHAMASISHA UPANDAJI MITI
Wanawake viongozi wa vyama vya ushirika kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani wamefanya zoezi la upandaji miti katika Shule ya Sekondari ya Bujingwa iliyoko Halmashauri ya Ilemela Mwanza.
Zoezi hilo limefanyika leo Februari 27,2025 likiongizwa na Mrajisi Msaidizi wa vyama vya ushirika Mkoa wa Mwanza Bi. Hilda Boniphace, amesema waletumia fursa hiyo ili kumuunga mkono Rais Samia kuhakikisha matumizi ya nishati safi yanakuwa endelevu.
"Tumekuja hapa kupanda miti ili kuwapa somo wanafunzi hao kutambua umuhimu wa utunzaji wa mazingira kukabiliana na tabia nchi,mpango ambao amekuwa akiuhimiza kiongozi wetu mkuu wa nchi," Hilda.
Amesema Kwa kuipa umuhimu unaostahili siku hiyo wameamua kufanya mambo yanayomgusa mwananamke, timu ya wanawake viongozi wa ushirika imewatembelea wanawake wenzao katika Halmashauri zote za Mkoa kianzia kuanzia Februari 24/2/2025 hadi 28/2/2025.
Halikadhalika Mrajisi huyo msaidizi amebainisha zoezi la kuwatembelea makundi ya Wanawake limekuwa na matokeo chanya kutokana na walivyohamasika kujiunga kwenye ushirika huku wakiwa na mpango wa kuanzisha Saccoss moja kubwa ya Wanawake.
Kauli mbiu ya maadhimisho haya ya *“Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji”*
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.