Wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 kwa Mkoa wa Mwanza wamekula kiapo cha uadilifu na usimamizi wa uchaguzi huo.
Akitoa maelezo kuhusu viapo hivyo Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza Mhe. Andrew Kabuka amewataka wasimamizi hao wa uchaguzi kuzingatia viapo na kufanya kazi hiyo kwa uadilifu na uaminifu mkubwa.
"Nimepewa jukumu la kuwaapisha wasimamisizi wa Serikali za mitaa nina imani kila mmoja anajua nini maana ya kiapo kwamba ukiishaapa unaahidi kufanya kazi kwa weledi,uaminifu na kwa kutunza siri kwa manufaa ya nchi yetu,"aliseme Kabuka.
Awali akifungua kikao hicho cha wasimamizi wa uchaguzi kula kiapo Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Christopher Kadio amewataka wasimamzi hao kuzingatia Kanunu za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa za mwaka 2019 na Mwongozo wa Uchaguzi ili kuhakikisha kazi hii ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa inafanyika kwa kufuata Kanuni na Mwongozo huo.
"Wasimamizi wa uchaguzi hawa tunawategemea sana kwa sababu ni nguzo ya kupata kile tunachokitegemea katika uchaguzi wa Serikali za mitaa,"alisema Kadio.
"Ni mategemeo yetu sote na mategemeo ya Ofisi ya Rais TAMISEMI kama mamalaka ya uchaguzi wa Serikali za mitaa kuwa wasimamizi hawa walioapishwa leo hii watashiriki katika Uchaguzi kwa Maslahi mapana ya Nchi yetu kama amani,demokrasia, mshikamano na umoja."alisema Kadio.
Hata hivyo Kadio amewakabidhi vitendea kazi ili waweze kufanya kazi yao kwa uadilifu ambavyo ni Nakala ya kanuni za Uchaguzi, na Mwongozo wa uchaguzi wa Serikali za mitaa ambapo uchaguzi huo utafanyika Novemba 24 mwaka huu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.