WATAFITI WA KILIMO WATAKIWA KUFANYA UWE NA TIJA KWA WAKULIMA
Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Mwanza Ndg. Peter Kasele ametoa rai kwa watafiti wa maswala ya kilimo kuhakikisha wanafanya utafiti wenye faida ili kuweza kutatua changamoto za mbegu kwa wakulima na kuimarisha sekta ya kilimo.
Ametoa rai hiyo leo Septemba 26, 2024 akimuwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza katika ukumbi wa Victoria palace wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya uzalishaji wa mbegu za vipando vya muhogo, viazi vitamu na migomba kwa njia ya haraka.
Amesema ujio wa teknolojia hiyo mpya ya uzalishaji wa mbegu italeta mabadiliko makubwa kwa wakulima na wananchi kwa ujumla na kuhakikisha usalama wa chakula na mazao.
"Kuja kwa hii teknolojia ni kama mkombozi kwa wakulima itasaidia kwa asilimia kubwa kuzalisha mazao kwa kiwango kikubwa ambapo tutakuwa na uhakika wa kuongeza usalama wa chakula". Amesema Kasele
Aidha amewataka wakulima nao kuwa tayari kuipokea teknolojia hiyo mpya ambayo inakuja kuleta mabadiliko katika kilimo na kuachana na teknolojia za zamani.
Naye mkurugenzi wa Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TIRA) Ukirigiru Dr. Paul Saidia amesema Taasisi ya TIRA inamchango mkubwa katika kusimamia na kuendesha shughuli za kilimo kwa wananchi na wakulima.
Mafunzo hayo yameandaliwa na Taasisi ya kilimo Tanzania (TIRA) na Taasisi ya kimataifa ya utafiti wa maendeleo (CIAT) ambazo zinatekeleza mradi wa kuboresha mfumo wa upatikanaji wa mbegu Bora za vipando Africa (PROSSIVA).
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.