WATAFITI WA ZAO LA PAMBA TUMIENI VYEMA FURSA YA KITAALAM KUTOKA BRAZIL-RC Makalla
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.CPA. Amos Makalla ameipongeza Serikali ya Brazil kupitia mradi wa BEYOND COTTON kwa msaada wa kitaalamu kwa zao la Pamba na kuwataka watafiti wa hapa nchini kutumia vyema nafasi hiyo ili zao hilo liwe na tija zaidi.
Akifungua leo kikao kazi cha pili kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa cha wadau hao kutoka Brazil Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Mhe.Hassan Masalla amebainisha kutokana na umuhimu wa zao hilo utafiti wa kitaalamu unahitajika zaidi ili mkulima azidi kunufaika na pato la Taifa kuongezeka.
Amebainisha kuwa mradi wa BEYOND COTTON unaokwenda pamoja na namna ya uzalishaji mazao ya lishe wenye gharama ya Shs bilioni 1.4 ukiwa na muda wa mwaka mmoja na nusu umewanufaisha wakulima wa Pamba zaidi ya elfu kumi kutoka Wilaya za Magu, Kwimba na Misungwi.
"Nimesikia kuna utaalamu unafanyiwa kazi wa kubakiza maji kwenye udongo,naamini watafiti wetu wakiufanyia utafiti wa kina kwa kushirikiana na wenzetu kutoka Brazil utakuja na matokeo chanya kwenye zao la Pamba",Mhe.Masalla.
"Tanzania tutazidi kupata Pamba bora na mazao ya lishe kupitia mradi huu na kuachana na kilimo cha mazoea, kwani tayari tumefanikiwa kupata vifaa vya kisasa vya kilimo cha zao hilo na uwezo wa kuwaangamiza wadudu waharibifu kama Chawakijani,"Marco Mtunga,Mkurugenzi Bodi ya Pamba.
Akizungumzia kuhusu utafiti Mkurugenzi wa Taasisi ya Kilimo Ukiliguru,Dkt.Paul Saidia amesema kupitia mradi huo umechangia ugunduzi wa mbegu bora na uwezo wa kupamba na magonjwa ya Pamba na ulimaji bora wa mazao ya nafaka na jamii ya mikunde.
Mradi wa BEYOND COTTON ulianza rasmi mwaka 2022 ukigharamiwa na Serikali ya Brazil ukilenga Wilaya za Magu,Kwimba na Misungwi zinazolima zao la Pamba kwa kuwajengea uwezo wa Kilimo cha kisasa pamoja na elimu ya mazao la lishe.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.