WATENDAJI WA HALMASHAURI WAASWA KUZINGATIA MAADILI NA SHERIA
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe. Hassan Masala ametoa rai kwa Watendaji wa Halmashauri kuzingatia kanuni, maadili na sheria ili kujenga mahusiano mema mahala pa kazi na kutoa huduma bora kwa jamii.
Amesema hayo mapema leo tarehe 04 Machi, 2025 wakati akifungua mafunzo ya Sheria kwa viongozi wa Halmashauri ya Ilemela na Nyamagana kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana yaliyoandaliwa na Wizara ya Katiba na Sheria.
Mhe. Masala amesema utawala kama mamlaka ni lazima yaendane na utoaji wa maamuzi yenye tija kwa kazini kwa kuzingatia misingi ya utawala bora hususani ushirikishwaji na uwazi kwenye maamuzi.
"Mafunzo haya yamekuja katika wakati muafaka kwani jamii yetu ina changamoto ya uelewa mdogo wa misingi ya haki za binadamu, uwepo wa mila na desturi kandamizi, vitendo vya ukatili wa kijinsia na tuhuma za ubakaji." Mhe. Masala.
Aidha, amewataka washiriki kwenda kuwa chachu ya mabadiliko kwenye jamii kwa kuhamasisha wananchi kudumisha amani na utulivu kwenye maeneo yao wakati wakitekeleza majukumu ya kujitafutia kipato.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.