WATUMISHI RS MWANZA WAANZA SAFARI YA KWENDA BWAWA LA UMEME MWL NYERERE
Watumishi 33 kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wameanza safari ya kwenda kutembelea Bwawa la Umeme la Mwl Nyerere lililopo mkoani Pwani ikiwa ni ziara ya kutembelea baadhi ya miradi mkubwa iliyowekezwa na Serikali.
Akizungumzia safari hiyo leo Februari 19, 2025 kiongozi wa msafara huo ambaye ni Afisa Utumishi Bw. Paul Cheyo amebainisha kuwa ziara hiyo itawaongezea watumishi hao ufahamu wa mambo mbalimbali yanayofanywa na Serikali na utalii wa ndani kwa jumla.
Ameongeza kuwa hii ni fursa nyingine ambayo pia itawaongezea watumishi ari ya kufanya kazi baada ya kupata nafasi ya kubadilsha mazingira.
"Tunatumia muda mwingi kutoa huduma kwa wananchi na wakati mwingine mtumishi anakosa muda wa likizo kutokana na kutingwa na majukumu, naamini ziara hii italeta mageuzi chanya watumishi watakaporudi kazini", amesema Cheyo.
Baadhi ya watumishi hao wakiwa na nyuso za furaha wametoa shukran kwa viongozi wao zkiwemo Mkuu wa Mkoa Mhe Said Mtanda na Katibu Tawala Balandya Elikana kwa kuwapatia nafasi hiyo na kuwaomba wazidi kuwa wabunifu zaidi kwa mambo yenye tija kwa wafanyakazi wakitolea mfano ziara hiyo.
"Hii kwangu ni ziara ya kwanza kulitembelea Bwawa la Umeme la Mwl Nyerere kwa kazi yangu ya kuhabarisha umma kuhusiana na taarifa za Serikali,ziara hii itaniongezea uelewa wa kutosha",Jacob Marcus,Afisa Habari.
"Nimefurahi pia kupata fursa ya kutembelea mradi wa Treni ya kisasa ya SGR na kusafiri nayo kutoka Dar hadi Dodoma,ni utalii wa ndani wa kujionea maeneo mbalimbali ya nchi yetu," Elizabeth Lupindo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.