WATUMISHI UKEREWE FANYENI KAZI KWA WELEDI KUEPUKA HOJA ZA KUJIRUDIA:RAS BALANDYA
Watumishi wa Halmashauri ya Ukerewe wametakiwa kufanya kazi kwa weledi na kutoa ushirikiano kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ili kuepuka hoja za kujirudia.
Akizungumza kwenye Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo lililokutana kujadili hoja za CAG za mwaka 2022/2023, leo juni 28 2023 Balandya amebainisha kumekuwa na kasumba ya kutompa ushirikano mzuri CAG na matokeo yake hoja kuchukua muda mrefu kumalizwa.
"Nawapongeza sana kwa kuwa na hati safi kwa miaka 3 mfululizo, sasa ongezeni bidii katika mapato ya ndani ili muweze kuwa na miradi yenye tija kwa wananchi". Balandya.
Aidha amewataka Madiwani kudhibiti na kusimamia vizuri miradi ya maendeleo ambayo itachangia kuongeza kipato na hali bora kwa wananchi
"Halmashauri ya Ukerewe katika hesabu za mwaka 2023 ilikuwa na hoja 30, huku hoja 18 zimemalizwa hoja 8 zipo hatua ya utekelezaji na 4 zimejirudia". John Mashimo, CAG.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe.Christopher Ngubiagai akitoa hotuba ya shukrani ameomba Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuongeza idadi ya watumishi ili kuongeza ufanisi wa kazi.
"Ndugu Katibu Tawala hapa Halmashauri tuna upungufu wa watumishi kwa 53% yupo mwamasheria mmoja tu akipata dharura mambo mengi yanakwama". Amesema Mkuu wa Wilaya.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.