Wavuvi wamehakikishiwa punguzo la tozo, ushuru wa mazao ya samaki na kodi kwenye zana za uvuvi waweze kunufaika.
Unafuu huo utapatikana baada ya mabadiliko ya sheria yatakapofanyika ili waweze kupata fursa ya kufanya biashara na kujipatia mapato .
Hayo yamebainishwa na Mjumbe wa kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wavuvi pamoja na wananchi wa kisiwa kidogo Gana kata ya Ilangala wilaya ya Ukerewe kwenye mkutano wa kampeni za mgombea Urais wa CCM, Dkt. John Magufuli.
Alisema wilaya ya Ukerewe asilimia 90 ya wakazi wake ni wavuvi hivyo serikali itaimarisha maeneo ya uvuvi kwa kupunguz ushuru wa samaki ambao kwa sasa ni sh. 300 ambayo wavuvi wameomba ifishuke na kubaki sh.100.
Alisema ushuru wa dagaa ni sh .100 kwa sasa lakini wameomba punguzo la sh.50 hivyo serikali yao imewasikiliza na inakwenda kubadilisha sheria ili wafanye biashara vizuri na kukuza vipato vyao.
Aliwaasa wavuvi kushirikiana na serikali kuhakikisha wanaimarisha sheria na kubadilisha maeneo yote yenye kero .
Akizungumza suala la kodi alisema wanaendelea kuodoa kodi zote hasa kwenye zana za uvuvi ,kuwaondolea ada ya leseni ya kuuza na kuvua samaki Ziwa Victoria watokanao na maji baridi, pia mchakato wa kuimarisha upatikanaji wa nyavu kwenye maduka unaendelea ili kuwasogezea huduma.
Kwenye kuondoa kodi tumeanzia kwenye vyavu,nyuzi zinazoshona nyavu, engine (mashine za kuoachika) zinazobebwa mkononi na kuwekwa kwenye mitumbwi,vifungashio kwa watu wa viwanda tunaendelea suala la upatikanaji wa nyavu kama kuna tajiri yeyote yupo huku hiyo ndio fursa anzisha duka la kuuza bidhaa za uvuvi na wewe tutakupunguzia kodi ,endeleeni kuiunga mkono serikali yenu na sisi hatutawaangusha"alieleza Majaliwa.
Aliongeza kuwa sekta ya Uvuvi imeimarishwa kwani huko nyuma walikuwa na migogoro , Ziwa Victoria linavuliwa na nchi tatu huku wavuvi wa nchi hizo wakituhumiwa kuwanyanganya samaki ,hatuwazuii lakini watuachie kila mmoja aende upande wake hivyo zoezi lile lilikuwa la kuwekana sawa,kutambuana ili wapangane vizuri na walifanikiwa.
Aliongeza kuwa wataleta boti kwa ajili ya makamanda ili kuimarisha ulinzi kwa wavuvi wakiwa ziwani Baada ya kukubwa na matukio ya wavuvi kutoka nchi zingine kuwavamia na kuwanyanganya bidhaa zao ,hivyo makamanda 67 wa maji watakuwa wanafanya kazi ulinzi.
" Zamani Wizara hii ilikuwa kubwa mno ilikuwa Kilimo, Mifugo na Uvuvi lakini Mhe. Dkt.John Magufuli ameitenga sasa ipo ya Uvuvi na Mifugo tu mambo yamekwenda kuratibiwa na tumeanza kukaa na wavuvi ili kurekebisha sekta hii tunachofanya sasa tunaunga makundi ya wavuvi ili kuweza kuwafikia tuweze kuyasikia matatizo yenu pia kazi tunayoifanya Sasa waziri wetu anapita kukutana na wavuvi kusikiliza na kuchukua changamoto zao ili ziweze kutatuliwa" alieleza Majaliwa.
Pia akizungumzia suala la vivuko alisema wanafufua meli zote za zamani ambazo zinakarabatiwa ili zifanye kazi hasa maeneo ya visiwani pia uimarishwaji na uboreshwaji wa vivuko unaendelea ,kukamilisha ujenzi wa vivuko vyote sambamba na ujenzi wa meli mpya kubwa ambayo inatarajiwa kuwa na uwezo wa kubeba abiria 1200,tani 400 za mizigo .
Pia Majaliwa alitoa ahadi ya kuwatatulia changamoto ya umeme,maji ,afya ,elimu pamoja na kufanya ukarabati wa shule,ujenzi wa mabweni na kuifanya ghana kuwa hadhi ya Kijiji kutoka kitongoji sambamba na kuwajengea Zahanati ili wananchi hao waweze kupata huduma hivyo wakichague chama cha mapinduzi kwani ndiyo yenye kuwaletea maendeleo zaidi .
" Tukishamaliza hizi pilikapilika ziara yangu ya kwanza itakuwa Ilugwa na Ghana kwani ndani ya miaka mitano nimeweza kufika huku pia mtambue kuwa mnayo haki ya kuchagua viongozi imara wenye uwezo wa kuongoza na kuisimamia serikali, tuna mambo mengi tumeyafanya lakini tunataka kuboresha zaidi."alieleza Mhe.Majaliwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.