WAWAKILISHI KONGAMANO LA KISWAHILI UGANDA WAKABIDHIWA BENDERA YA TAIFA MWANZA
Leo Aprili 11, 2025 Wawakilishi wa Mkoa wa Mwanza wanaotarajiwa kuiwakilisha Tanzania katika Kongamano la Kiswahili litakalofanyika nchini Uganda kuanzia tarehe 14 hadi 16 Aprili 2025, wamekabidhiwa bendera ya Taifa leo katika makabidhiano maalum yaliyofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Makabidhiano hayo yamefanywa na Bw. Peter Kasele ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa na amewataka kuiwakilisha vyema Tanzania kwa uzalendo umahiri na uhodari wa lugha ya Kiswahili.
Kongamano hilo ni sehemu ya utekelezaji wa Dira ya Kiswahili 2025 - 2050 inayolenga kukuza na kuimarisha matumizi ya Kiswahili kama lugha ya mawasiliano, elimu, biashara na utangamano katika ukanda wa Afrika Mashariki na Bara zima.
Wawakilishi hao kutoka Mwanza wataungana na washiriki wengine kutoka nchi mbalimbali, wakitarajiwa kuchangia mijadala na shughuli zitakazoweka msingi wa mustakabali wa Kiswahili katika kizazi kijacho.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.