WAZIRI JENISTA AWASILI MWANZA KUSHIRIKI SIKU YA KUPIGA VITA DAWA ZA KULEVYA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama leo Juni 29, 2024 amefika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Said Mtanda ofisini kwake, aliyefika Mkoani humo kushiriki maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupiga vita dawa za kulevya inayotarajiwa kuadhimishwa Juni 30, 2024 Jijini Mwanza.
Mhe. Jenista amewasili Mwanza akiwa ameambatana na Naibu Waziri wake Mhe. Ummy Nderiananga pamoja na Katibu Mkuu Dkt. Jim Yonaz
Mara baada ya mazungumzo mafupi Mhe. Jenista pia amepata fursa ya kuzungumza na wanamdahalo kuhusu athari na namna ya kujikinga na matumizi ya dawa za kulevya, mdahalo uliofanyika kwenye ukumbi uliopo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Aidha Waziri Jenista pia amepata fursa ya kutembelea na kukagua mabanda mbalimbali ya maonesho katika viwanja vya nyamagana ambapo pia ametoa vyeti vya ushiriki kwa wadau mbalimbali.
Maadhimisho ya mwaka 2024 yanaongozwa na kauli mbiu isemayo "Wekeza kwenye Kinga na Tiba Kudhibiti Dawa za Kulevya" ambapo inasisitiza elimu kwa jamii ili iweze kufahamu madhara ua dawa za kulevya na kushirikisha jamii katika kutatua changamoyo zinazotokana na dawa za kulevya.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.