WAZIRI KIKWETE ATOA ZAWADI KWA SHULE/WALIMU WALIOFANYA VIZURI KITAALUMA MWANZA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete ameipongeza Serikali ya Mkoa wa Mwanza kwa kujiwekea mkakati mzuri wa kuzipongeza halmashauri, walimu na shule za msingi na sekondari zilizofanya vizuri katika mitihani ya kujipima ya Mkoa.
Ametoa pongezi hizo wakati akizungumza na wakuu wa shule pamoja na wadau wa elimu katika kikao kilichofanyika kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza leo Septemba 26, 2024,na kuongeza kuwa motisha hiyo iwe chachu ya kufanya vizuri zaidi.
Aidha Mhe. Kikwete amezipongeza Halmashauri za Kwimba na Sengerema kwa kufanya vizuri na kuongoza Halmashauri zingine kwenye mitihani ya kujipima ya Mkoa kwa shule za msingi na sekondari,kitendo ambacho kinaonesha kumuunga mkono kwa vitendo Mhe.Ris Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye ametoa fedha nyingi katika sekta ya elimu nchini
"Kwa upekee kabisa niipongeze sana wilaya ya kwimba na Sengerema kwa kuvunja rekodi ukiachilia wilaya za Ilemela na Nyamagana ambazo ndio zilikua zikishindana lakini mwaka huu wamepata ushindani". Amesema Mhe. Kikwete wakati akizungumza na na viongozi hao
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza na Afisa elimu kukaa na kupanga mikakati ya motisha za juu lengo likiwa Mkoa huo uzidi kung'ara katika ufaulu wa wanafunzi kuanzia kimkoa hadi Taifa.
"Maafisa elimu chini ya Katibu Tawala wakakae waboreshe nyaraka hii inayoonesha mkakati wa Mkoa katika kuboresha elimu halafu tuweke siku maalumu na wadau wa elimu ya kuuzindua kuelekea mwaka 2025". Amesema Mhe. Mtanda.
Kikao hicho cha utoaji wa zawadi kwa Halmashauri, Walimu na shule za sekondari na msingi kimeambatana na zoezi la kukabidhi madawati Arobaini (40) kwa shule ya Msingi Uhuru iliyopo Wilaya ya Nyamagana kata ya Igoma iliyokabiliwa na upungufu huo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.