Waziri Mchengerwa aagiza miradi ya afya Sengerema ianze kutoa huduma haraka
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Mhe. Mohamed Mchengerwa ameagiza vituo vya afya vilivyopo wilayani Sengerema vianze kutoa huduma haraka kwa wananchi.
Akizungumza leo kwenye kituo cha afya kilichopo kijiji cha Kanyerere kilicho chini ya mradi wa Tasaf kilichofika asilimia 96 lakini hakijaanza kutoa huduma, Waziri Mchengerwa amesema haoni sababu ya msingi ya kuwacheleweshea huduma wananchi licha ya kupewa maelezo ambayo hayakumridhisha.
Amebainisha maelezo yote aliyopatiwa kuhusu kituo hicho yameonesha waliopewa dhamana ya kusimamia wameshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo hivyo ametoa wiki mbili kituo hicho na vingine 11 viwe vimeanza kutoa huduma.
"Katibu Tawala wa Mkoa nakuagiza simamia ipasavyo zoezi hili waandikie barua wahusika wote ili mradi huu uanze kazi,hatuna sababu ya kuwapa hasira wananchi wetu kituo wanakiona lakini wanaendelea kuteseka kupata hudum seea za afya,"Mhe Mchengerwa.
"Mhe Waziri kwa mujibu wa taratibu za Tasaf mradi huu wananchi walitakiwa kuchangia asilimia 10 na Tasaf asilimia 90,sasa kuna baadhi ya vijiji vimesua sua kuweka nguvu zao ndiyo maana mradi huu umechelewa kuanza kwa wakati,"Binuru Shekidele,Mkurugenzi Halmashauri ya Sengerema.
"Kituo hiki kimegharimu shs milioni 481 kuna upungufu wa shs milioni 35 ili kiweze kutoa huduma kwa wananchi,bado hatujaingiza umeme na maji,"Malisa Ndugha,mratibu wa Tasaf ,Sengerema
Mbunge wa Jimbo la Sengerema Mhe.Hamis Tabasamu amesema bado baadhi ya vijiji wanafunzi wanalazimika kutembea umbali wa km 18 kwenda shule, amehakikishiwa na Waziri Mchengerwa shule zote zilizoanzishwa kwa nguvu ya wananchi jimboni kwake na zimeishia hatua ya boma Serikali itazigharamia kuzikamilisha.
Waziri Mhe Mohamed Mchengerwa aliyesimama kwa muda mfupi wilayani Sengerema akitokea Mkoani Geita kuja Mwanza, amesema Serikali imeunda timu ya wakaguzi wa miradi ya elimu na afya watakaozunguka nchi nzima kufanya tathmini ya miradi hiyo na kutoa ushauri kwa Setikali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.