WAZIRI MKUU AMUAGIZA MENEJA WA TANROADS KUHAKIKISHA BARABARA ZA MAGU ZINAPITIKA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) amemuagiza Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) kuhakikisha barabara zote Wilayani Magu zinapitika ili ziendane na kasi ya ukuaji wa Wilaya hiyo.
Mhe. Waziri Mkuu ametoa agizo hilo mapema leo Desemba 21, 2024 mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa daraja jipya la Sukuma (70m) na barabara unganishi (2.294) kupitia barabara ya Magu Mahaha Mkoani Mwanza.
Mhe. Majaliwa amesema Serikali inaendelea na juhudi za kuwaletea wanananchi wake maendeleo ambapo katika mradi huo zaidi ya bilioni 9 zimetolewa ili kurahisisha huduma ya usafirishaji na kukuza uchumi wa wananchi wa Wilaya ya Magu na Mkoa wa Mwanza kiujumla.
“Hapa nimeridhishwa na kazi iliyofanywa na Mkandarasi mzawa, natoa rai kazi hii ikamilike kwa wakati kwani Magu sasa inakwenda kukua kwa kasi na miundombinu hii lazima ikamilike ili iendane na kasi hiyo”.
Aidha Mhe. Majaliwa amesema Magu ni sehemu ya fursa ya kibiashara na uchumi na kuwasihi wananchi wa Wilaya hiyo kuanza kampeni ya kuchagiza maendeleo kwani Mwanza sasa ineshakuwa na hakuna nafasi tena.
Awali akisoma taarifa ya mradi huo Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Mhomamed Besta amesema daraja jipya la Sukuma litakuwa na urefu wa mita 70 na upana wa mita 11.35 na litajengwa umbali wa mita 800 pembeni ya daraja la zamani kwenye uelekeo wa mto huku likitekelezwa na Mkandarasi mzawa Mumangi Construction Ltd na anatarajia kukamilisha mradi huo juni 05, 2025.
Akihitimisha ziara yake wilayani Magu Waziri Mkuu amekagua ujenzi wa daraja la Mto simiyu (Mita 175) na barabara Unganishi (KM 3) lenye thamani ya Tshs. Bilioni 48 lenye upana wa Mita 12.3 na ameagiza kasi ya ujenzi ili aprili 25, 2025 litakamilike na kuondoa adha ya daraja finyu lililojengwa kabla ya uhuru.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.