Zaidi ya Wakufunzi 400 Mkoani Mwanza wamehitimu mafunzo ya Sensa ya Watu na Makazi tayari kwenda kutoa mafunzo kwa makarani
ngazi za Wilaya ikiwa ni maandalizi ya zoezi hilo la Taifa litakalofanyika Agosti 23 2022.
Mafunzo hayo ya siku 21 yaliyofanyika Chuo Kikuu cha Mt. Agustino yamefungwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe Mhandisi Robert Gabriel huku akiwataka mafunzo yao yaje na majibu chanya wakati wa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi litakapofanyika.
"Sisi tuna imani nanyi kwenda kufanya kazi iliyo bora ya uelimishaji ili Wananchi wapate uelewa na kushiriki vyema muda utakapofikia" Mkuu wa Mkoa.
Amesema ili Taifa lisonge mbele ni lazima lijue matakwa halisi ya Wananchi wake ili mikakati ya huduma kama vile Elimu,Maji,Hospitali na nyinginezo ziwe bora na za uhakika.
"Natoa pongezi za dhati kwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa muongozo wake imara kwa Taifa letu ambao una malengo ya kutuletea Maendeleo" Mhe Gabriel.
Mratibu wa Sensa ya Watu na Makazi Mkoani Mwanza,Goodluck Lyimo amebainisha Wakufunzi hao wamepata uelewa wa kutosha muda wote wa Mafunzo hayo yakiwemo utumiaji wa Madodoso yote manne ya Sensa hivyo watakuwa sehemu ya mafanikio ya zoezi hilo.
Sensa ya Watu na Makazi itafanyika Agosti 23 mwaka huu kwa wale wote watakaolala ndani ya mipaka ya Tanzania.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.