Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli jumatatu atashuhudia utiaji saini wa mikataba ya ujenzi wa meli mpya, chelezo na ukarabati wa meli za MV.Victoria na MV.Butiama.
Hafla hiyo itafanyika katika eneo la Bandari ya Kusini (Mwanza South Port) kata ya Igogo jijini Mwanza semptemba 3, 2018.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella alisema, Rais atashuhudia utiaji saini wa mikataba hiyo kati ya wakandarasi na Wizara husika, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku mbili mkoani hapa inayoanza semptemba 3 hadi 4.
Mongella alisema, ukarabati wa meli hizo wanatarajia kuchukua hata miaka miwili na kuajiri watu takribani 400,sanjari hayo jumanne septemba 4 Dkt.Magufuli atazindua viwanda vitatu katika kijiji cha Isangijo wilayani Magu.
Alisema, siku hiyo hiyo atazindua mradi wa upanuzi wa Chuo cha Ualimu Murutunguru wilayani Ukerewe na baadaye mradi wa maji katika kijiji cha Nebuye wilayani humo.
Aidha, mbali na hayo atapata fursa ya kuhutubia wananchi wa wilaya ya Ukerewe kupitia mkutano wa hadhara utakaofanyika katika uwanja wa Gertrude Mongella Nansio.
Hata hivyo aliwaomba wananchi kujitokeza kumlaki Rais na kumuunga mkono kwa kufanya kazi ili kukuza uchumi wa mtu binafsi, wilaya,mkoa na taifa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.