• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Uchapakazi wa vijana kwenye Kilimo Ukerewe wamridhisha Mgumba

Posted on: July 25th, 2019


Serikali imevutiwa na uchapakazi wa vijana wilayani Ukerewe ikisema jambo ni tofauti na wilaya nyingine kwa sababu vijana wengi hawataki kuwekeza kwenye kilimo na hata waliowezeshwa kuanzisha miradi ya maendeleo, mingi imekufa kwa kukosa matunzo.

Kauli hiyo ilitolewa  na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe.Omari Mgumba wakati akizungumza na kikundi cha vijana wa Kata ya Bugorola wilayani humo baada ya kuonyesha kuridhishwa na kuvutiwa na mradi wa umwagiliaji wa kikundi hicho cha vijana na kwamba hakuna mtu kutoka nje atawaletea maendeleo.

Alisema vijana wengi hawako tayari kuwekeza kwenye kilimo badala yake wamekuwa wakikimbilia mijini na kuwaacha wazee vijijini wakiendesha kilimo, tofauti na Wilaya ya Ukerewe ambako vijana wanajituma na kuchapa kazi kwa kulima mazao mbalimbali  na kufanya shughuli za uvuvi na ufugaji.

Mgumba alisema malengo ya Serikali ni kuona wananchi wanalima kwa tija ili kuongeza vipato vyao na kuinuka kiuchumi kupitia sekta ya kilimo, hivyo vijana ambao ni nguvu ya taifa watumie fursa hiyo na kuyatumia mabonde yaliyopo wilayani humo kwa kilimo chenye tija.

“Nimevutiwa na jinsi mnavyomuunga mkono Mhe.Rais John Magufuli na serikali yake kupitia kauli mbiu yake ya "Hapa Kazi Tu".Vijana wanawaacha wazee na kuhamia mijini lakini hapa Ukerewe vijana mnachapa kazi , mnalima pilipili hoho, mahindi,nyanya na mazao mengine .Mnajituma katika kilimo mazao, mifugo, uvuvi na misitu na kutunza mazingira na kuwawezesha kupata kipato na kuinuka kiuchumi,”alisema.

Akizungumzia  chanzo cha maji cha mradi wa umwagiliaji wa Bugorola Naibu Waziri huyo wa Kilimo alisema una mchango mkubwa wa maendeleo kwenye sekta ya kilimo lakini kwa sasa ni chakavu  kutokana na miundombinu yake kuwa ya muda mrefu na haukidhi tena mahitaji.

“Mradi huu kwa mujibu wa sheria  umechakaa sana kwa sababu ni wa muda mrefu tangu ujengwe mwaka 1974, kuukarabati ni gharama kubwa  pia mahitaji makubwa yameongezeka ambapo umekufa kwa kukosa matunzo kwani inahitaji kutunzwa ili iwatunze lakini ikifa itaonekana hamna nia serikali iwasaidie, hivyo wataalamu watakuja kufanya tathmini ya mahitaji ili fedha za kuuboresha ziletwe,”alisema Mgumba.

Aliongeza kuwa kazi ya serikali ni kuwajengea uwezo,  haina fedha za matunzo na matengenezo ya mundombinu ya  ya miradi ya umwagiliaji na kuwataka vijana 21 kati ya 100 wa mradi wa kilimo cha umwagiliaji Bugorola kuonyesha mfano kwa wengine kwa kuchapa kazi ambapo serikali itawaunganisha na masoko ya uhakika wa mazao yao.

Alieleza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imeamua kufanya mapinduzi kwenye sekta ya kilimo ili wakulima walime kibiashara badala ya kilimo cha kujikimu ambapo imeanzisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) kwa ajili ya kuwakopesha wakulima mitaji na matrekta.

Awali Ofisa Umwagiliaji wa Wilaya ya Ukerewe, Emil Sirwamba alimweleza Mhe. Mgumba kuwa kina cha maji cha mradi wa Bugorola kiko mbali na mfumo wake unatakiwa kubadilishwa ambapo eneo linalotumika kwa kilimo kwa sasa  ni hekta 74  tu kati ya hekta 200 na kuiomba serikali iongeze fedha au ijenge chanzo na mfumo mpya.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mradi wa Vijana Bugorola,Nicolaus Kusanya alisema kikundi hicho kiliundwa na vijana 100 lakini wamebaki 21 na kwamba wanakabiliwa na changamoto ya nishati ya mafuta kwa ajili ya kuvuta maji kutoka ziwani na kujaza kwenye tenki.

Diwani wa Kata hiyo Domician Mnyoro alisema changamoto kubwa ya kundi hilo la vijana wanaohangaika na kilimo ni ukosefu wa mitaji na pembejeo hivyo serikali iwasaidie na isisite kuwapa fursa zingine zinapopatikana.  

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.